108 - MGAWANYIKO WA WATU KATIKA WAHYI (UFUNUO)

عن أبي موسى الأشعريِّ، عن النبيِّ ﷺ قال:«مَثَلُ ما بعَثَني اللهُ به من الهُدى والعِلم، كمَثَل الغَيث الكثيرِ أصاب أرضًا: فكان منها نَقِيَّةٌ، قبِلَت الماءَ، فأنبتَت الكَلَأَ والعُشبَ الكثير، وكانت منها أجادبُ، أمسكت الماءَ، فنفعَ اللهُ بها الناسَ، فشَرِبوا وسَقَوْا وزرعوا، وأصابت منها طائفةٌ أخرى، إنما هي قِيعانٌ لا تُمسِك ماءً ولا تُنبتُ كلأً، فذلك مثَلُ مَن فَقُه في دِين الله، ونفَعه ما بعَثَني الله به فعَلِم وعَلَّم، ومَثلُ مَن لم يرفَعْ بذلك رأسًا، ولم يَقبَلْ هُدى الله الذي أُرسِلْتُ به» متفق عليه.

Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash-Ariyy (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema,

1. Mfano wa aliyonituma kwayo Allah (s.w) miongoni mwa uongofu na elimu, ni kama mfano wa mvua nyingi iliyonyesha katika Ardhi Fulani, 

2. Ikawa Ardhi hiyo ni safi ikapokea maji na kuotesha mazao na mimea. 

3. Na ikawa sehemu nyingine ni kavu ikapokea maji, na Mwenyezi Mungu akawanufaisha watu kwa mvua hiyo wakanywa na wakanywesheleza mifugo na wakalima mazao. 

4. Na ikanyesha sehemu nyingine ya ardhi, hakika sehemuhiyo ni jangwa halihifadhi maji na wala halioteshi mimea  

5. Basi huo ni mfano  wa mtu aliopewa utambuzi katika dini na mwenyezimungu akamnufaisha na yale aliyonitumanayo kwayo, akayatambua na akawaelimisha watu wengine,na mfano wa Yule ambaye  hakuyapa kipaumbele wala hakukubali mwongozo wa mwenyezimungu ambao nimetumwa kwao.(Imepokelewa na Imam Bukhari na Muslimu).

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

Na ardhi njema, yenye udongo wa rutba, hutoa mimea yenye kukua vizuri yenye uhai, kwa idhini ya Mola Mlezi wake. Na ardhi mbaya haitoi ila mimea michache, isiyo na faida, tena kwa shida. Na hivyo ndivyo tunavyo zipambanua Ishara (Aya) kwa watu wanao shukuru.

[Surat Al-A'raf: 58].

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia

Nitawatenga na Ishara zangu wale wanao fanya kiburi katika nchi bila ya haki. Na wao wakiona kila Ishara hawaiamini. Wakiiona njia ya uwongofu hawaishiki kuwa ndiyo njia; lakini wakiiona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndiyo njia. Hayo ni kwa sababu wamezikanusha Ishara zetu, na wameghafilika nazo.

[Surat Al-A'raf: 146]

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia

Mfano wa makundi mawili ni kama kipofu na kiziwi, na mwenye kuona na Anasikia. Je, wawili hawa wanakuwa sawa kwa kufananishwa? Basi, je, hamfikiri? .

[Surat Hud: 24]

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia

Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu yaliyo kusanyika juu yake. Na kutokana na wanavyo yayusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyo piga mifano ya Haki na baat'ili. Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo piga mifano..

[Surat AR-RAA'D: 17]

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia

124. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.   125. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? 126. (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa.  .

[Surat Taha: 124-126]

Halikadhalika Mwenyezi Mungu mtukufu amesema

43. Na hiyo ni mifano tunawapigia watu, na hawaifahamu ila wenye elimu.

[Surat Al-Ankabut: 43]

Miradi ya Hadithi