1. Anapiga picha Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake hali za watu juu ya kuipokea na kuikubali elimu ambayo alikuja nayo Mtume (s.a.w), akaifanya elimu hiyo ni kama mvua nyingi ambayo ndani yake kuna manfaa (faida) kwa ajili ya watu, Na akataja Mtume (s.a.w) mvua kwakua watu wanaihitajia sana , kama ambavyo kupitia ,mvua ardhi inapata uhai(uzima), basi vilevile elimu kwani Mwenyezi Mungu (s.w) huzihuisha nyoyo kwa elimu.
Na hakika zimetofautiana athari za mvua kwa kutofautiana na halihalisi ya ardhi ambayo imenyeshelezewa na mvua, kama ilivyopiga picha juu ya jambo hilo hadithi tukufu.
2. basi aina ya kwanza katika ardhi: safi, nzuri yenye rutuba, haina majanga, ni bora zaidi kwa kilimo, mvua imenyesha juu ya ardhi hiyo basi ardhi ikanywa vema maji ya mvua hiyo, na ikaotesha mimea-nayo ni jumla ya mimea inayoota ardhini- na nyasi-nayo ni uoto mbichi-, basi ikanufaika Ardhi pindi ilipopata uhai kwa maji, na ikanufaisha wengine pindi ilipo otesha vile ambavyo anakula mwanaadamu na wanyama wengineo.
3. Aina ya pili ya ardhi: ardhi ngum ambayo sio nzuri sana kwa kilimo, hainywi maji haraka, bali inayahifadhi maji, basi ardhi hiyo hainufaiki kwa maji hayo katika kilimo, na si vinginevyo wananufaika watu kwa ardhi hiyo pindi yanapokusanyika maji ya mvua, basi wanakunywa katika maji hayo na wananywesha wanyama wao na kumwagilizia mazao yao.
4. Na aina ya tatu: Jangwa; yaani: Ardhi iliyosawasawa tambalale, haifai kwa kilimo, wala haitunzi (hifadhi) maji, nyenyewe haikunufaika kwa maji na haikurutubika na haikuotesha, wala watu hawakunufaika kwa ardhi hiyo kwa kunywesheleza au kilimo.
5. Kisha akatafsiri Mtume wa Mwenyezi Mungu hiyo hali: basi akataja kwamba aina ya kwanza ni Wanazuoni, ambao walifahamu- na neno fiqhu: Ni kuelewa na kutambua-makusudio ya Mwenyezimingu na Makusudio ya Mtume wake (s.a.w), wakayafanyia kazi na wakawafundisha watu wengine. Na aina ya pili: wao wanakua ni njia na sababu ya kuifikisha elimu japokua sio katika watambuzi, na aina ya tatu: Ni wale ambao hawakuyakubali aliyokuja nayo Mtume Muhammad (s.a.w) hawakuyahifadhi wala hawakuyafikisha kwa wengine, wala hawakuyafahamu na hawakuyafanyia kazi. Na hawa ndio Makafiri na Waovu ambao wametupilia mbali sheria na mwongozo wa Mwenyezi Mungu (s.w).
1. Alikua Mtume (s.a.w) ni mbora watu wote kimafunzo, na mwenye uwezo mkubwa wa kubainisha, na alikua na pupa na hamasa juu kuwaongoza watu, basi akapita njia zote kwa ajili ya kufikisha wito wa mola wake, nayeye hapa: anapiga mifano ya wazi (inayoonekana); kwani kufanya hivyo inaweka karibu maana za kiakili na inasaidia katika kuelewa na kupata maarifa, basi nijuu ya kila mlinganiaji atumie nyezo ambazo zitarahisisha kuelewa kwake na kufuata kwake mafundisho.
2. Hitajio la watu kwenye Elimu kama hitajio la Ardhi kwenye Mvua au zaidi, basi liwe jambo la kwanza ambalo watu wanaomba uokovu kupitia hilo, na litawanufaisha kwalo, na litawatolea huduma na matumizi kwa hilo:ni kusomesha dini ya Mwenyezi Mungu (s.w).
3. Elimu inaota na kumea katika nyoyo nzuri kama ambavyo Nyasi zinastawi katika ardhi nzuri, basi anaetaka Elimu basi asafishe moyo wake kutokana na majanga ya ushirikina na hasadi na kutokujali kwa upumbavu, na arudi kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.
4. Katika jambo hilo, amesema ibn taymiyat:” Hakika moyo unapokua mwepesi na mlaini, basi unakua kupokea kwake elimu ni rahisi na wepesi na elimu hutulia ndani yake, na inathibiti na ina athiri, na ukiwa msusuavu wenye vifundo, unakua (moyo huo) kupokea kwake elimu ni kuzito na kugumu. Na lazima pamoja na hayo uwe mtakasifu, msafi, tena ulio salimika ili iwe safi pia elimu ndani yake na uzae matunda mazuri, Na kama si hivyo kama utapokea elimu na ikawa ndani yake kuna uchafu na ubaya, utaharibu uchafu hiyo elimu, na inakua kama ugonjwa katika mazao, ikiwa haukuzuia mbegu kuota, basi huzuia mmea kustawi na kupendeza, na jambo hili liko wazi kwa wenye macho ya mazingatio” [1].
5. Daraja la juu zaidi kwa mwenye kukusanya elimu na matendo pamoja na kusomesha wengine, ni kama ile ardhi nzuri iliyopokea maji na ikaotesha nyasi kwa ajili ya wengine, na wao wako juu ya daraja kutokana na kiwango cha bidii yao, basi wakajitahidi katika kuyatimiza hayo yote.
6. Mtu yeyote Ambaye hakuweza kuwa mwanazuoni basi ahamishe elimu kwa watu wake.
Na hakika amesema Mtume Muhammad (s.a.w):
“fikisheni kwa niaba yangu japo aya moja” [2]
. Na huwenda jambo hilo likawa na manfaa zaidi kutoka kwenye ufahamu wao na mafundisho yao pekee,
ni kama maneno ya Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake:
“Basi alioko hapa amfikishie ambaye hayupo, kwani huenda yule atakae fikishiwa akawa ni mwenye kuhifadhi zaidi na kuyafanyia kazi kuliko aliye yasikia” [3]
nayeye anashiriki katika malipo (thawabu) kwa Yule anaemhamishia elimu.
7. Muda wowote utakapoona uzito katika nafsi yako juu kuukubali mwongozo wa Mwenyezi Mungu (s.w) na mwongozo wa Mtume wake (s.a.w) na kupambana nao kwa midahalo: basi irejee nafsi yako, na uisafishe kutokana na kibri na pumbazo, na uchukuwe tahadhari usiwe miongoni mwa wale watu aliowaelezea Mwenyezi Mungu mtukufu: “Nitawapotosha na kuwaweka mbali na hoja (dalili) zangu ambao wanafanya kiburi katika ardhi pasina haki ya kufanya hivyo,na wanapoona hoja na dalili zangu hawazikubali,na wanapoona njia ya uongofu hawaifanyi ni njia ya kufuatwa, na wanapoona njia ya upotevu wanaifanya kua ni njia ya kufuatwa, hayo ni kwa sababu wao wamekanusha na wamepinga hoja (dalili zetu) na wakawa kunako hoja hizo ni wenye kughafilika” [4] .
8. Amesema mshairi:
Watu bora ni wale waliopewa elimu, kwani wao ni waelekezi kwa wenye kutafuta uongofu.
Na thamani ya mtu hutokana na yale ananyoyatenda vizuri, na wasiojuwa huwa ni maadui wa wenye elimu.
Basi simama imara katika elimu wala usitafute badala, kwani watu wote ni wafu na wenye elimu hubaki hai.
8.Amesema mwingine:
Kuwa katika watu ni msomi au mwenye kutafuta elimu = au msikilizaji mzuri kwani elimu ni vazi la kifahari
jifunze kitu katika kila fani wala usiwe mjinga asiejua chochote = kwani mtu huru hufahamu mambo mengi.
Marejeo
- Majmuu’ al-Fatawa (9/315, 316).
- Al-Bukhari (3461), kutoka kwa Abdullah bin Amr bin Al-Aas, Mungu awe radhi nao.
- Al-Bukhari (1741), kutoka kwa Abu Bakra, Mungu amuwiye radhi.
- Al-Bukhari (1741), kutoka kwa Abu Bakra, Mungu amuwiye radhi.