عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ لِمُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ حِينَ بَعَثَهُ إِلَى اليَمَنِ: «إِنَّكَ سَتَأْتِي قَوْمًا أَهْلَ كِتَابٍ، فَإِذَا جِئْتَهُمْ، فَادْعُهُمْ إِلَى أَنْ يَشْهَدُوا أَنْ لا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ اللَّهَ قَدْ فَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ اللَّهَ قَدْ فَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً تُؤْخَذُ مِنْ أَغْنِيَائِهِمْ فَتُرَدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَإِيَّاكَ وَكَرَائِمَ أَمْوَالِهِمْ، وَاتَّقِ دَعْوَةَ المَظْلُومِ؛ فَإِنَّهُ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَ اللَّهِ حِجَابٌ» متفق عليه


Kutoka Ibn Abbas (r.a) amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake, kumwambia Mua’dh ibn Jabal wakati alipomtuma kwenda yemen:

1. “Hakika wewe utawaendea watu wa kitabu 2. Utakapo waendea, walinganie kwenye shahada wakiri kwa moyo kuwa hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye peke yake, na hakika Nabii Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. 3. Ikiwa watakukubalia hilo, basi waeleze kwamba hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhishia sala tano mchana na usiku. 4. Ikiwa watakukubalia hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewafaradhishia juu yao, zaka ya mali zao, inachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na inapelekwa kwa maskini wao.  5. Ikiwa watakukubalia hilo, basi jiepushe na kuchukua malizao bora zaidi. 6. Na ogopa duwa ya aliye dhulumiwa, kwani hakika hakuna kati yake na Mwenyezi Mungu pazia” . Imepokelewa na Bukhari na Muslimu. 

Abu Al-Abbas, Abdullah Bin Abbas Bin Abdul-Muttalib

Ni: Abu Al-Abbas, Abdullah Bin Abbas Bin Abdul-Muttalib, Al-Qurashi, Al-Hashimi Alizaliwa kwenye “Sha’ab Bani Hashim” miaka mitatu kabla ya kuhama, alikuwa ni marabi wa taifa na mfasiri wa Qur’an, binamu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie na alikuwa akiitwa: Bahari; kutokana na ujuzi wake; Mtume rehma na Amani zimshukie alimuombea dua kwa kusema: “Ewe Mola Mpe ufahamu wa Dini. [1] Na ni miongoni mwa maswahaba waliopokea hadithi nyingi sana, alisilimu akiwa mdogo sana, na alishikamana na Mtume Amani iwe juu yake baada ya kufunguliwa mji wa makka na akasimulia kutoka kwake. Alipoteza uwezo wa kuona mwishoni mwa maisha yake, na alifariki huko Taif katika mwaka wa 68 Hijiria. [2]

Marejeo

1.  Imepokewa na Al-Bukhari (6732) na Muslim (1615)

2. Imepokewa na Al-Bukhari (143) na lafudhi ni yake, na Muslim (2477).

Miradi ya Hadithi