عَنْ أَبِي ذَرٍّ رضي الله عنه أَنَّ نَاسًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ ﷺ قَالُوا لِلنَّبِيِّ ﷺ: يَا رَسُولَ اللهِ، ذَهَبَ أَهْلُ الدُّثُورِ بِالْأُجُورِ، يُصَلُّونَ كَمَا نُصَلِّي، وَيَصُومُونَ كَمَا نَصُومُ، وَيَتَصَدَّقُونَ بِفُضُولِ أَمْوَالِهِمْ، قَالَ: «أَوَلَيْسَ قَدْ جَعَلَ اللهُ لَكُمْ مَا تَصَّدَّقُونَ؟ إِنَّ بِكُلِّ تَسْبِيحَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَكْبِيرَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَحْمِيدَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةً،  وَأَمْرٌ بِالْمَعْرُوفِ صَدَقَةٌ، وَنَهْيٌ عَنْ مُنْكَرٍ صَدَقَةٌ، وَفِي بُضْعِ أَحَدِكُمْ صَدَقَةٌ»قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، أَيَأتِي أَحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أَجْرٌ؟ قَالَ: «أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَهَا فِي حَرَامٍ، أَكَانَ عَلَيْهِ فِيهَا وِزْرٌ؟ فَكَذَلِكَ إِذَا وَضَعَهَا فِي الْحَلَالِ كَانَ لَهُ أَجْرٌ».

Kutoka Kwa Abu Dharr, Mwenyezi Mungu awe radhi naye 1- Kwamba maswahaba walimwambia Mtume rehma na Amani zimshukie: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Watu wenye mali wamekwenda na ujira wao mkubwa, wanaswali tunaposwali, wanafunga sisi tunapofunga, na wanatoa sadaka kutokana na fedha zao za ziada. 2- Akasema Mtume: Je! Mwenyezi Mungu hakukufanyieni sadaka mnazotoa? 3- Kumtakasa Mwenyezi Mungu ni sadaka, kila kumtukuza ni sadaka, kila neno la kumsifu ni sadaka, na kila tahlili ni sadaka. 4- Kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka. 5- Na katika ndoa ya mmoja wenu kuna sadaka. 6- Wakasema maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, vipi mmoja wetu akidhi matamanio yake kisha apate ujira ?  Akasema Mtume: “Je, mnaonaje kama akiyaweka matamanio hayo kwenye haramu atapata dhambi ?” Basi akifanya katika halaali anapata thawabu"


Muhtasari wa Maana

Baadhi ya masahaba masikini walimlalamikia Mtume rehma na amani ziwe juu yake kwamba matajiri wamepata fadhila na vyeo vya juu kupitia sadaka zao, basi Mtume rehma na Amani zimshukie akawaambia wana kheri katika matendo yanayochukua nafasi ya ujira wa sadaka.

Miradi ya Hadithi