عَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ «مَا بُعِثَ نَبِيٌّ إِلَّا أَنْذَرَ أُمَّتَهُ الأعْوَرَ الكَذَّابَ، أَلا إِنَّهُ أَعْوَرُ، وَإِنَّ رَبَّكُمْ لَيْسَ بِأَعْوَرَ، وَإِنَّ بَيْنَ عَيْنَيْهِ مَكْتُوبٌ "كَافِرٌ" 

Kutoka kwa Anas Mwenyezi Mungu awe eradhi naye amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie:

“Hakutumwa Nabii ila aliwaonya watu wake kutokana na mwongo wenye jicho moja.Fahamu kuwa ni mwenye jicho mojaNa Mola wako Mlezi si mwenye jicho moja.Na baina ya macho yake imeandikwa neno “kafiri”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

“Hakika wale ambao neno la Mola wako Mlezi limekwisha thibitika juu yao, hawataamini (96) Ijapo kuwa itawajia kila Ishara, mpaka waione adhabu iliyo chungu”

[Yunus: 96, 97].


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Lakini Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma”

[At-Tawbah: 128].

Miradi ya Hadithi