Taabiiyu mkubwa ambaye ni, Tariq bin Shihab, Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu, ametaja kuwa Marwan bin Al-Hakam ndiye aliyekuwa wa kwanza kutanguliza khutba kabla ya Swalah ya Idi, Inajulikana katika dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba Swalah ya Idi inafanyika kabla ya khutba, isipokuwa Marwan aliogopa watu kuondoka baada ya Swalah, hivyo akataka kuwahutubia kabla ya kuondoka [1]Basi mtu mmoja akasimama ili kumnasihi na kumwonyesha Sunnah, ambayo ni kwamba Swalah ndio kwanza, kisha khutba. Marwan hakumjibu mshauri, na akamwambia: Watu wameacha unayoyasema.
Wakati huo Abu Said Al-Khudri, radhi za Allah zimshukie, alisema: Ama mtu huyu ambaye alimnasihi Marwan, alifanya wajibu wake kutoa nasaha na kuamrisha mema na kukataza maovu, hivyo uwajibu kwake ukaondoka. Kama ambavyo Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi juu ya uwezo wake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema:
“Haimlazimu Mtume ila kufikisha ujumbe tu.”
Kisha akatoa ushahidi Abu Said Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutokana na yale aliyoyasikia kutoka kwa Mtume rehma na Amani zimshukie pale aliposema: “Mwenye kuona ubaya miongoni mwenu, na uovu ni kila kitu Sharia imekikemea na inakichukia - na aibadilishe kwa mkono wake mwenyewe."
Kuibadilisha kwa mkono haina maana kwamba Muislamu aharakishe kuharibu pesa na vitu na kumwaga damu, kwani hiyo itakuwa ni sababu ya fitna na kukabiliwa na madhara na maudhi. Bali, inatakiwa kubadili kwa mkono, kuwepo uwezo wa kufanya hivyo bila ya kuwepo madhara, na hiyo ni sawa na yule mwenye mamlaka anayebadili kwa mamlaka yake anachokikana, na kama baba na mume anayewatia adabu watoto wake na kushutumu familia yake. Ikiwa hawezi kuibadilisha kwa mkono, ataomba msaada kwa imamu na wasaidizi wake ili kuibadilisha, vinginevyo kukemea kwa mkono kunakuwa hakuna nafasi kwake.
4. Ikiwa mtu hawezi kubadili uovu kwa mkono wake mwenyewe; Kwamba akiogopa madhara kwake au fitna atakazozifanya, basi atahamia hatua ya pili ambayo ni kukemea kwa Ulimi. Ambayo ni kumkemea yule aliyefanya maasi kwa uasi wake, na kumlingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumhimiza kutubu na kuuondoa uovu huo, kwa kutumia njia nzuri ya kumfikishia mhusika, iwe ulaini au ukali, kwa mujibu wa kauli yake Mola mlezi na mtukufu!
“Waite kwenye njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema”
5. Akiogopa na hawezi kukataza ubaya kwa mkono wake, basi alaani kwa moyo wake; Kwa kuuchukia uovu huo, kuukana kwa Mwenyezi Mungu, na kuazimia kwamba kama angeweza kuubadilisha, angeukemea.
Na kukemea uovu moyoni ndio daraja dhaifu ya imani, kwani hakuna baada ya kuchukia moyoni ila mtu anastarehe na dhambi na kutosheka nayo hata asipoifanya, na kwa ajili hiyo ikaja katika simulizi nyingine: “Kinyume na hayo hakuna chembe ya imani”[2]
Kuamrisha mema na kukataza maovu ni miongoni mwa faradhi. Ni kwa manufaa ya jamii na kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu. Ni faradhi ya kutoshelezeana, kama baadhi wakifanya hivyo, basi dhambi huondolewa kwa waliobakia, isipokuwa itakuwa ni faradhi ya lazima kwa mtu endapo uovu huo hakuna aliye uona aua kuujua, au ikiwa uovu uko miongoni mwa watu wa nyumbani mwake na anayesimamia mambo yao[3]
Na shari ikiwa ni katika mambo ambayo hukumu yake inadhihirika kwa watu wote, kama vile kuacha Swalah, saumu, kuwaasi wazazi, unywaji wa pombe, uzinzi na mengineyo, basi kila Muislamu ana wajibu wa kukemea hilo. Lakini ikiwa ni miongoni mwa mambo ambayo hukumu yake haiko wazi kwa kila mtu, basi kulizuia hilo ni kwa wenye elimu.
Mafunzo
Katika Hadithi, kuna ishara isemayo kwamba mwenye kuingiza kitu katika Dini kisicho kuwemo, basi amali zake zitakataliwa, na kwamba amali hazikubaliwi isipokuwa zikiwa sambamba na mwongozo wa Mtume rehma na amani zimshukie.
Yule mtu aliyetoka kumnasihi Marwan bin Al-Hakam hakuogopa dhulma na uwezo wake, na akampa nasaha. Muislamu hatakiwi kuogopa kukemea maovu maadamu hajafikia kile ambacho kitasababisha madhara.
Kusikuzuie kujua kwako kwamba huyo utakae mkemea hatakusikiliza, Unachotakiwa kufanya ni kushauri, na Mungu humwongoa amtakaye.
Kamwe usifikiri kwamba kujiepusha na dhambi kunatosha kukuokoa na adhabu. Hakika kutokukemea maovu kunakuwajibisha adhabu; Amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: “Watu wakiona uovu na wasiubadilishe, basi Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa adhabu yake”[4]
Haijuzu kwa Muislamu kuona ubaya na anauwezo wa kuubadilisha halafu akaacha bila ya kuukemea, Amesema Allah mtukufu :
“Walilaaniwa walio kufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka (78) Walikuwa hawakatazani maovu waliyo kuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyo kuwa wakiyafanya”
Tahadhari na kubadilisha uovu kwa kuleta uovu mkubwa kuliko, bali unapaswa kutumia hekima unapokemea uovu, ukiona kukemea kwa ulimi kuna faida zaidi kuliko kubadilisha kwa mkono, basi fanya hivyo.
kubadilisha uovu kwa kutumia mkono kunahitaji uwezo wa kubadilika na usalama wa madhara na fitna. Ukitimiza masharti fanya hivyo.
Miongoni mwa kukemea kwa mikono, ni Mwislamu kutokukubali mke wake, binti yake au dada yake atoke nje akionyesha mapambo yake, katika hali hiyo haitoshi kwake kumnasihi bali ni lazima azuiwe kufanya hivyo na hata kwa mkono.
Ni sehemu ya kukemea maovu kwa mkono wakati ambao Muislamu anawaamrisha jamaa zake kuswali na kuabudu, na kutoa adhabu kwa yale anayodhania kuwa yatakuwa sababu ya kuongoka.
Ni miongoni mwa kukemea uovu kwa mkono, Muislamu kuondoa nyumbani kwake alama za ushirikina na dhambi. kama vile picha, sanamu, hirizi, na kadhalika.
Iwapo huwezi kubadilisha kwa mkono na ukaweza kushauri na kueleza ukweli kwa hekima bila fitnah au madhara, basi fanya hivyo.
Kubadilisha uovu kwa kutumia ulimi si kwa kutukana, kukashifu, au kusengenya, bali ni kwa kutoa nasaha, kuamrisha mema kwa haki, na kukataza maovu bila ya ubaya.
Muislamu mkweli ni lazima aharakishe kuamrisha mema na kukataza maovu, na hazuiliwi kufanya hivyo na khofu ya wenye vyeo vya juu katika dunia hii. Mwenyezi Mungu akasema:
“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu”
Kuamrisha mema na kukataza maovu hakuishii kwa Viongozi na watawala. kwa hakika ni wajibu kwa Waislamu binafsi; Ni wajibu kwa Muislamu kuamrisha na kukataza, maadamu anajua anachoamrisha na anacho kikataza.
Katika kumhurumia mwislamu aliyeasi na kuihurumia jamii kiujumla ni kutoa nasaha na kuzuia mikono yake.
Muumini wa kweli haridhiki na kujirekebisha tu; Bali anabeba shida za umma unaomzunguka, na anafanya kazi ya kubainisha hatari zinazowatishia katika dini yao na dunia yao.
Moja ya balaa kubwa kwa mtu ni kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu ili kupata mapenzi ya mpenzi, jamaa, urafiki wa rafiki, au kujipendekeza kwa mtawala; Laana iliwashukia Wana wa Israili pale kitu kama hicho kilipowazuia kuamrishana mema na kukatazana maovu.
Iwapo Muislamu hataweza kukemea kwa maneno, ni lazima achukie moyoni mwake, aichukie dhambi hiyo, aiweke kwa Mwenyezi Mungu, na aazimie kwamba kama angeweza kuikemea kwa mkono wake au kwa ulimi wake, basi angefanya hivyo.
Miongoni mwa kukemea kwa moyo ni kutokuwa na hatia ya ushirikina na watu wake; Kwa hivyo Muislamu anapaswa kuwachukia washirikina na makafiri, na wala hafanyi urafiki nao na kuwafanyia urafiki kwa yale wanayoyafanya katika suala la chuki yao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na chuki yake kwao.
Ujaribu moyo wako na imani; Ukiuona ubaya na ukaukanusha kwa mkono, ulimi au moyo, basi una imani kiasi cha kukemea uovu. Na usipojali hilo, jua kwamba uko mbali na bustani za Waumini.
kukemea kwa moyo huku ukiwa na uwezo wa kukemea kwa mkono au ulimi ni udhaifu katika imani ya mja, basi jitahidi kuwa miongoni mwa watu wenye imani kamili.
Kukaa kwako katika mikusanyiko ya pumbao, kusengenyana, kuteta, na mambo ya haramu kunaashiria kuwa moyo wako haukemei uovu. Kama ungekuwa ukikemea uovu, basi ungechukia mkusanyiko huo na kuwa mbali nao.
Marejeo
- Tazama: “Kashf al-Mushkil min Hadeeth al-Sahihayn” cha Ibn al-Jawzi (2/173).
- Imepokewa na Muslim (50).
- “sherh ya Arobaini ya Nawawi” cha Ibn Daqeeq Al-Eid (uk. 112).
- Imepokewa na Ahmed (1), Ibn Majah (4005), Abu Dawood (4338), na Al-Tirmidhi (3057).