17 - KULAZIMIANA NA KUMFUATA MTUME MUHAMMAD

عن الْمِقدامِ بنِ مَعْدِي كَرِبَ رضى الله عنه أن النبيَّ قال: «ألا هل عسى رجُلٌ يَبْلُغُه الحديثُ عَنِّي وهو مُتَّكِئٌ على أريكته، فيقول: بينَنا وبينَكم كتابُ الله، فما وجدْنا فيه حلالًا استَحْلَلناه، وما وجدْنا فيه حرامًا حرَّمناه، وإنَّ ما حرَّمَ رسولُ الله ﷺ كما حرَّمَ اللهُ». وفي لفظ أبي داودَ: «ألا إني أوتيتُ الكتابَ ومثلَه معه».


Kutoka kwa Al-Miqdaam bin Maadi Karb, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema:

“Je, inawezekana kwa mtu kumpa khabari ya Hadithi kutoka kwangu akiwa ameegemea kiti chake, na akasema: Baina yetu na nyinyi kuna Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi chochote tunachokikuta humo ni halali tunaihalalisha, na tunayoyakuta ndani yake kuwa ni haramu tunayaharamisha.Aliyoharamisha Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam nayo ni haramu kwa Mwenyezi Mungu.”Kwa kauli ya Abu Daawuud: “Nimepewa Kitabu (Qur`an)  pamoja na mfano wake ”.

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema”

[An-Nisa: 59].

Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 “Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao”

[An-Nisa: 80].

Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 “Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri”

[An-Nahl: 44].

54. Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume. Na mkigeuka, basi yaliyo juu yake ni aliyo bebeshwa, na yaliyo juu yenu ni mliyo bebshwa nyinyi. Na mkimt'ii yeye mtaongoka. Na hapana juu ya Mtume ila kufikisha Ujumbe wazi wazi”

[An-Nur: 54].

Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 “Wala hatamki kwa matamanio (3) Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa”

[An-Najm: 3, 4].

Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 “Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho.”

[Al-Hashr: 7].

Miradi ya Hadithi