عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ قَالَ اللَّهُ: «أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لا عَيْنٌ رَأَتْ، وَلا أُذُنٌ سَمِعَتْ، وَلا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ»، فَاقْرَؤوا إِنْ شِئْتُمْ: ﴿فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ﴾ [السجدة: 17].

Kutoka kwa Abu Hurayrah, radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie amesema:

Mwenyezi Mungu amesema: “Nimewaandalia Waja wangu wema yale ambayo jicho halijaona, Hakuna sikio lililosikia, Haijatokea kwenye moyo wa mwanadamu. Someni maneno ya Mwenyezi Mungu: “Basi hakuna nafsi yoyote inayojua waliyo tunziwa na kufichiwa katika faraja na tulizo la macho yao” [Al-Sajdah: 17].

  1. Hii ni Hadith iliyopokelewa na Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu mbali na Qur’ani Tukufu, na mfano wa hadithi hii huitwa Hadithil Qudsi:

  2. Mola wetu Mlezi, Ametakasika na Ametukuka, Anafahamisha kwamba Amewaandalia waja wake wema, malipo ya utiifu wao na ibada yao ambayo hawaja pata kuona mfano wake, Hawakuweza kuona chochote chenye jina kama lake. Kama miti, mito, majumba ya dhahabu na fedha, lulu nzuri na mengineyo, pamoja na uzuri wa watu wake, na mandhari nyinginezo.

  3. Pia Peponi kuna sauti nzuri ambayo hawajaisikia, kama vile kuimba na sauti nyinginezo, na pia kuna habari ambazo hawajasikia mfano wake.

  4. Kisha akathibitisha kwamba Alicho kitayarisha hakiwezi kujulikana kwa mtu yeyote. Ikiwa mja hajaona wala kusikia, na zote mbili ni hisia za utambuzi, basi hawezi kufikiria kwa akili yake ukweli wa neema hizo. Inapoingia katika fikra za mja aina mbalimbali ya neema, starehe, na mapambo, kamwe hatafikia uhalisia wa neema hiyo ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu amewatayarishia waja wake wema.

  5. Na akaongeza uthibitisho wa hilo kutokana na maneno yake yaliyoteremshwa, Akasema: Soma ukipenda:

    “Basi hakuna nafsi yoyote inayojua waliyo tunziwa na kufichiwa katika faraja na tulizo la macho yao, hayo ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda”

    [Al-Sajdah: 17].

    ” Maana yake: Hakuna nafsi inayojua kile ambacho Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaandalia na kuwafichia waja Wake walioamini katika Pepo miongoni mwa aina za neema, furaha, na wema mwingi ambao macho hupendezwa nayo na kufurahishwa nayo.

Pepo na neema zake zimetajwa mara kwa mara ndani ya Qur-aan, ndiyo maana Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Mahali pa kuhifadhia mkwaju –mjeledi- peponi ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake. Hiyo” [1].

Mafunzo

  1. Mapenzi makubwa zaidi ni kuwapenda watu wema kwani wao wako pamoja na Mwenyezi Mungu: “Anawapenda na wao wanampenda” [Al-Ma’idah: 54] Wanamuandalia matendo ya utiifu - na anajitosheleza - na anawaandalia yale ambayo jicho halijaona, sikio halijasikia, na moyo wa mwanadamu haujaingia. Kuweni pamoja na watu wema, na wakati wowote mnapokuwa wavivu katika njia ya Mwenyezi Mungu basi kumbuka makazi ambayo Mwenyezi Mungu Mkarimu ametayarisha kwa watu wema.

  2. Al-Hasan, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Watu walificha vitendo katika dunia, basi Mwenyezi Mungu akawafichia yale ambayo jicho halijaona wala sikio halijasikia” [2]. Ikiwa ndivyo hivyo, basi Muislamu anapaswa kuhesabu ibada zake za siri ambazo hakuna anaezijua isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye aliye mfichia hizo kheri nyingi zisizo na mfano kwa kuonwa na kutazamwa. 

  3. Pepo ipo hivi sasa, na Mwenyezi Mungu ameitayarisha kwa ajili ya watu wema miongoni mwa waja wake, basi dunia ikikuletea starehe mbalimbali zilizoharamishwa, basi iambie nafsi yako: Pepo ipo tayari, na hakuna chochote ila ni kusubiri muda mfupi tu ili kuifikia na kuingia.

  4. Watu wengi hujisemea kuhusu starehe za dunia, na kuziwazia na kuzitamani. Pamoja na kwamba starehe zote za dunia na wanayoyawazia hayalingani na shibri moja ya peponi, basi mwenye akili timamu anatakiwa mara kwa mara kuikumbuka pepo, na yale ambayo Mwenyezi Mungu ametayarisha ndani yake ili ayatamani.

  5. Hebu wewe, familia yako na jamaa zako muwe mkuikumbuka Pepo na sifa zake, na kuwakumbusha watu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amerahisisha njia za kuelimisha na mawasiliano mbalimbali ambayo ni rahisi kufanya hivyo.

  6. Furaha kubwa kabisa peponi: ni kumuona Mwenyezi Mungu; kwa kuwa hawakumuona duniani, Amesema Allah aliyetakasika:

    “Zipo nyuso siku hiyo zitakazo ng'ara (22) kwa kumwangallia Mola wao Mlezi”.

    [Al Qiyama: 22, 23]

     na kutoka kwa Jarir bin Abdullah Radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) na akautazama mwezi usiku –mwezi kamili – akasema: “Hakika mtamuona Mola wenu, kama mnavyouona mwezi huu, hamtasongamana katika kumuona” [3] na adhabu kubwa zaidi watakayo adhibiwa watu waovu ni kunyimwa kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu. Amesema Mola mlezi:

    “Hakika ya watu waovu siku ya kiyama watazuiliwa kumuona Mola wao Mlezi.”

    [Al-Mutaffifin: 15]

  7.  Mshairi alisema:

Tenda matendo mema kwa ajili ya nyumba ya milele mlizni wake ni ridhaa = jirani wa nyumba hiyo ni Muhammad (s.a.w) na Mwenyezi Mungu ndio mjenzi wa nyumba hiyo. 

Nchi imejengwa kwa dhahabu na miski ndio udongo wake, na madini ya zafarani ndio magugu yanayoota ndani yake.

Mito yake ni ya maziwa safi na asali = na mvinyo hutiririka katika vijito vyake.

Mwenye kununua nyumba katika pepo ya al-Firdaws anaijaza = kwa rakaa moja anayoisali usiku giza linapotanda.

au kuondosha njaa kwa masikini = siku aliyozidiwa na njaa kali.

Marejeo

  1. Al-Bukhari (3250).
  2. Tafsir al-Kashshaf cha al-Zamakhshari (3/513).
  3. Al-Bukhari (554) na Muslim (633).


Miradi ya Hadithi