عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ قَالَ اللَّهُ: «أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لا عَيْنٌ رَأَتْ، وَلا أُذُنٌ سَمِعَتْ، وَلا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ»، فَاقْرَؤوا إِنْ شِئْتُمْ: ﴿فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ﴾ [السجدة: 17].

Kutoka kwa Abu Hurayrah, radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie amesema:

Mwenyezi Mungu amesema: “Nimewaandalia Waja wangu wema yale ambayo jicho halijaona, Hakuna sikio lililosikia, Haijatokea kwenye moyo wa mwanadamu. Someni maneno ya Mwenyezi Mungu: “Basi hakuna nafsi yoyote inayojua waliyo tunziwa na kufichiwa katika faraja na tulizo la macho yao” [Al-Sajdah: 17].

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Kwa wafanyao wema watalipwa mazuri na nyongeza nono. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala hawata pata udhalili. Hao ndio watu wa Peponi. Humo watadumu milele”  

[Yunus: 26].


Na akasema:

“Basi hakuna nafsi yoyote inayojua waliyo tunziwa na kufichiwa katika faraja na tulizo la macho yao, hayo ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda (17) Ati aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawezi kuwa sawa (18) Ama walio amini na wakatenda mema, watakuwa nazo Bustani za makaazi mazuri. Ndio pa kufikia kwa waliyo kuwa wakiyatenda” (19)

[Al-Sajdah: 17-19].


Pia amesema Mwenyezi Mungu:

“Huu ni ukumbusho Na hakika wachamungu wana marejeo mazuri (49) Bustani za milele zitazo funguliwa milango yake kwa ajili yao (50) Humo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji (51) Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao (52) Haya ndiyo mliyo ahidiwa kwa Siku ya Hisabu (53) Hakika hii ndiyo riziki yetu isiyo malizika” (54)

[Swaad.: 49-54].


Amesema Mola Mtukufu:

  “Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi je hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao ?”

[Muhammad: 15].

Miradi ya Hadithi