عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه  قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «لا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقْبَضَ العِلْمُ، وَتَكْثُرَ الزَّلازِلُ، وَيَتَقَارَبَ الزَّمَانُ، وَتَظْهَرَ الفِتَنُ، وَيَكْثُرَ الهَرْجُ - وَهُوَ القَتْلُ القَتْلُ - حَتَّى يَكْثُرَ فِيكُمُ المَالُ فَيَفِيضَ»

Kutoka kwa Abu Hurayrah Mwenyezi Mungu amuwiye radhi amesema: Amesema Mtume Rehma na Amani zimshukie:

“Hakitakuja kiyama mpaka Elimu iondolewe.Na matetemeko ya ardhi yaongezeke.Na wakati uwe mfinyo.Na ugomvi –fitna- zitadhihiri.Kuongezeka Machafuko - ambayo ni mauaji, kuuwana -Na kuongezeka mali na zitakuwa nyingi”

  1. Mtume, Rehema na Amani zimshukie, anataja baadhi ya alama ndogo za Kiyama, na akataja miongoni mwazo kuondolewa kwa elimu, ambayo ni kwamba Elimu inanyanyuliwa na kuondolewa ardhini kwa kufa wanazuoni wengi na kutokuwepo mtu wa kuwarithisha elimu zao na kuwa badala yao.

  2. Na moja ya alama za kiyama pia ni kwamba matetemeko yataongezeka na kuenea katika ardhi, nayo ni mitetemeko inayojulikana sana, ambayo matokeo yake ni maangamizi kulingana na nguvu inayopatikana katika mitikisiko hiyo na udhaifu wa vinavyo tikiswa.

  3. Miongoni mwa Aayah zake pia ni kwamba wakati utakaribiana, hivyo umri utapungua, na muda wa nyakati zinazojulikana utapungua, hivyo mwendo wa nyakati unaongezeka kulekea safari ya Kiyama, kwa mujibu wa makadirio ya Mwenyezi Mungu Mtukufu anayejua. Kama alivyosema Mtume: "hakitatokea kiyama mpaka muda utakapokaribiana, Kwa hivyo mwaka utakuwa kama mwezi, na mwezi utakuwa kama wiki, na wiki itakuwa kama siku. Na siku hiyo itakuwa kama saa moja, na saa itakuwa kama kiasi tu cha kuwasha  moto” [1]

  4. Miongoni mwa ishara za kiyama ni kuongezeka fitina kwa kiasi kikubwa sana, kama alivyosema Mtume Rehma na Amani zimshukie: “fanyeni haraka kutenda Matendo mema kabla haijakujieni fitina na mtihani, fitina hiyo ni kuchanganyika haki na batili na itakuwa vigumu mtu kutofautisha kati ya hizo mbili, hiyo fitina hiyo ni kama mfano wa usiku wa giza kali ambalo mtu hawezi kutofautisha yaliyomo katika giza hilo, hivyo watu watakuwa katika mkanganyiko, mpaka mtu aweza kuamka akiwa na Imani lakini jioni ikamkuta ni Kafiri ,au akashinda ni Kafiri lakini asubuhi ikamkuta yuko katika Imani kutokana na uzito wa majaribu, Vile vile kutokana na uzito wa majaribu hayo ni kwamba mtu ataacha Dini yake kwa ajili ya bidhaa duni tena ya bei mbaya ambayo ni Dunia”. [2]

Na Mtume, rehema na amani zimshukie, akaeleza kwamba fitina na mitihani itaongezeka zaidi karibu kabisa na kiyama, kiasi ambacho Muumini atatamani kifo kutokana na ukali wa mitihani katika dini ya Mwenyezi Mungu. Kama alivyosema Mtume rehema na amani zimshukie: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, dunia haitaondoka mpaka itafikia mtu aende kaburini, na atagalagala na kujigeuza juu yake huku akisema: Afadhali mimi ndio ningelikuwa ndali ya kaburi hili, na kutamani huko si kwamba amefanya kheri nyingi katika dini isipokuwa atatamani hali hiyo kutokana na dhiki na mitihani atakayokuwa akiiona wakati huo” [3]

5.   wa wingi wa fitna itadhihiri dalili nyengine ya kiyama ambayo ni wingi wa machafuko ambayo ni kuua, basi watu wataliona ni jambo la kawaida au kuua kwa kusudi kutaongezeka. Na Mtume amani iwe juu yake alibainisha kwamba kumuua Muislamu bila ya haki ni miongoni mwa madhambi Saba yenye kuangamiza [4], na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamuahidi adhabu Mwenye kuua kwa kusema:

“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.”

[An-Nisa: 93]

6.   Jambo la mwisho alilotaja Mtume Rehma na Amani zimshukie ni kuongezeka fedha katika Dunia mpaka watu au wengi wao watazikinai, na pengine tajiri asipate mwenye kuikubali Sadaka yake, amesema Mtume Rehma na Amani zimshukie: “jitoleeni katika mali zenu kabala haijafikia zama ambazo mtu atatembea na Sadaka yake ili kumpa mtu, basi atasema yule aliyepewa Sadaka hiyo, kama ungeniletea hii sadaka siku ya jana ningeliipokea, lakini kwa sasa sina shida nayo, na hakuna mtu atakayeweza kuikubali.”[5].

Mafunzo

  1. Hadithi hii ni miongoni mwa dalili za utume wake Rehma na Amani zimshukie; Alisimulia ishara nyingi ambazo nyingi katika hizo tayari zimepatikana, basi kila unapoona uthibitisho wa hilo katika maisha, jivunie dini yako na ongeza imani yako.

  2. Mtume Rehema na Amani zimshukie, Kuelezea yatakayotokea zama zamwisho katika mitihani na misukosuko huo ni muongozo kwa Muislamu ili awe na ufahamu katika hilo, na awe na tahadhari juu ya mitihani hii yenye kutokea zama hizo. Utakapo isikia tu, jiulize: Napaswa kufanya nini ili kufikia makusudio ya Mungu Mwenyezi?

  3. Moja ya alama za kiyama ni kuondolewa elimu na kuenea ujinga, na watu wengi wajinga na watu wa kawaida huthubutu kutoa fatwa na kusema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya kujua. Basi jihadhari na kushirikiana nao katika hayo, na chagua mtu mzuri ambaye utachukua kutoka kwake Elimu na Dini, wala usiwaogope wajinga, au jambo hilo likakupelekea kuto kuwapinga. Hayo ni mitihani ya Mwenyezi Mungu.

  4. Waislamu watafute na wajitahidi kutafuta elimu, na waandae misingi ya kuihifadhi, kwani elimu bado inachukuliwa kidogo kidogo, jambo ambalo linaongeza haja ya elimu na watu wake.

  5. Ukiona au kusikia matetemeko ya ardhi, basi haya yawe ni ukumbusho wa Akhera.

  6. Iwapo kupungua kwa Umri ni miongoni mwa alama za kiyama, basi mja afanye haraka kutubia na aharakishe kutenda mambo ya kheri kabla ya kushitukizwa na kifo, au kupungua fursa za ibada na utiifu, na hapo Baraka zinakosekana. 

  7. Muislamu lazima ashikamane na dini yake, na ajihadhari na kujiingiza katika fitna na matamanio. Bali anapaswa kuyakemea kadiri awezavyo; katika Hadith Mtume Rehma na Amani zimshukie amesema: “Mitihani na Fitina zitaingizwa kwenye mioyo kamavile mikeka, kijiti kwa kijiti. Moyo wowote utakaoikubali fitina, huandikwa ndani yake alama nyeusi, na moyo wowote utakaoipinga na kuikataa fitina, huandikwa ndani yake alama nyeupe, hivyo kutakuwa na nyoyo za aina mbili; nyoyo nyeupe kama mng’ao mweupe sana, aina hii ya nyoyo haitasumbuliwa na fitina au mitihani ya aina yoyote kwa muda wote ambao mbingu na ardhi zitadumu. Na aina nyingine ya nyoyo ni nyeusi sana katika sehemu nyeupe sana inayometa-meta, kama koni, hizi ni zile nyoyo ambazo hazijui mema na wala hazikemei maovu, isipokuwa kufuata matakwa na matamanio yake” [6].

  8. Sunnah ya Mtume Rehma na Amani zimshukie ilikuwa ni kujikinga na misukosuko, pia aliwaamrisha maswahaba zake wajikinge na hayo yote; Kutoka kwa Zaid bin Thabit, Mwenyezi Mungu awe radhi naye kwamba Mtume Rehma na Amani zimshukie amesema: “Jikingeni kwa Mwenyezi Mungu kutokana na fitina, iwe ya dhahiri au ya siri”[7]

  9. Miongoni mwa sababu za mauaji mengi: ni kutojali na kutojua hasara yake, hiyo hutokana na udhaifu wa dini, pia kutawaliwa na ubinafsi, au kulindana kwa kigezo cha kabila na nchi, ikiwa ni pamoja na mashindano yaliyoharamishwa katika pesa na wanawake, kufanya uzembe katika matumizi ya silaha zinazosababisha kifo, na idadi kubwa ya yale ambayo vijana wanayashuhudia katika hukumu zao, kama Kuuana katika sinema na michezo, kukabiliana na yote hayo ni wajibu wa kila mtu.

  10. Wingi wa pesa na ongezeko la watu katika maisha: Sio dalili ya zama Nzuri, kwani zama za Mtume Rehma na Amani zimshukie ilikuwa ni kipindi bora zaidi, Hakukuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya hivyo, kwa maana wakati unaohitajika kuwa bora ni ule ambao umejaa uadilifu.

  11. Amesema Mshairi:

Tunaishi hali ya kuwa Mwenyezi Mungu ametukusanya = lakini tutapokufa kiyama pia kitatuunganisha. 

Hujapata kuona kila saa katika muda = kuna tukio ambalo husababisha kifo. 

Ewe Mwenye kuimarisha dunia, fahamu kuwa unamjengea mwingine = Ewe Mwenye kuikusanya dunia, fahamu kuwa unamkusanyia mwingine.

Ninaona mtu anaikimbilia kila fursa katika dunia = lakini mtu afanye afanyavyo kuna siku atakufa.

Ametakasika yule ambaye hakuna Mfalme isipokuwa yeye = ni lini yatakamilika mahitaji ya asiyetosheka?

Marejeo

  1. Al-Tirmidhiy (2332).
  2. Muslim (118).
  3. Muslim (157).
  4. Al-Bukhari (2766), na Muslim (89),kutoka kwa Abu Hurairah
  5. Al-Bukhari (1411), na Muslim (1011), kutoka kwa Haritha bin Wahb
  6. Muslim (144).
  7. Muslim (2867).


Miradi ya Hadithi