عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِ‍يَّ ﷺ: أَيُّ الْعَمَلِ أَحَبُّ إِلى اللَّهِ؟ قَالَ: «الصَّلاةُ عَلى وقْتِهَا»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «ثُمَّ بِرُّ الْوَالِدَيْنِ»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «الجِهَادُ في سَبيل اللهِ» قَالَ: حَدَّثَنِ‍ي بِهِنَّ، ولَوِ اسْتَزَدْتُهُ لَزَادَنِ‍ي. 

Kutoka kwa Abdullah bin Masoud, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, ambaye amesema:

1. Nilimuuliza Mtume rehma na amani zimshukie: Ni amali gani anayoipenda zaidi Mwenyezi Mungu? Alisema: “kusali kwa wakati.” 2. Akasema: Kisha ipi? Akasema Mtume: “Basi waheshimuni wazazi.” 3. Akasema: Kisha ipi? Akasema Mtume Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu”. 4. Akasema: Alinieleza hayo tu, na lau ningeomba zaidi, angeniongeza.


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu: “Hawawi sawa Waumini wanao kaa tu wala hawanadharura, na wale wanao pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Mwenyezi Mungu amewatukuza cheo wale wanao pigana kwa mali yao na nafsi zao kuliko wale wanao kaa tu.” .

[An-Nisa: 95]

Na Mwenyezi amesema: “Hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu”.

[An-Nisa: 103]

Kisha akasema pia: “Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa” .

[At-Tawbah: 111]

Pia amesema aliyetukuka:

“Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima (23) Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni” .

[Al-Israai: 23, 24]


Miradi ya Hadithi