عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِ‍يَّ ﷺ: أَيُّ الْعَمَلِ أَحَبُّ إِلى اللَّهِ؟ قَالَ: «الصَّلاةُ عَلى وقْتِهَا»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «ثُمَّ بِرُّ الْوَالِدَيْنِ»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «الجِهَادُ في سَبيل اللهِ» قَالَ: حَدَّثَنِ‍ي بِهِنَّ، ولَوِ اسْتَزَدْتُهُ لَزَادَنِ‍ي. 

Kutoka kwa Abdullah bin Masoud, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, ambaye amesema:

1. Nilimuuliza Mtume rehma na amani zimshukie: Ni amali gani anayoipenda zaidi Mwenyezi Mungu? Alisema: “kusali kwa wakati.” 2. Akasema: Kisha ipi? Akasema Mtume: “Basi waheshimuni wazazi.” 3. Akasema: Kisha ipi? Akasema Mtume Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu”. 4. Akasema: Alinieleza hayo tu, na lau ningeomba zaidi, angeniongeza.


Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anatueleza kuwa matendo yanayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu na yaliyo karibu naye zaidi ni kuswali kwa wakati wake, kisha kuwaheshimu wazazi wawili, kisha kupigana jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Miradi ya Hadithi