عَنْ أَبِي مَالِكٍ الْأَشْعَرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ «الطُّهُورُ شَطْرُ الْإِيمَانِ، وَالْحَمْدُ للهِ تَمْلَأُ الْمِيزَانَ، وَسُبْحَانَ اللهِ وَالْحَمْدُ للهِ تَمْلَآنِ - أَوْ تَمْلَأُ - مَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ، وَالصَّلَاةُ نُورٌ، وَالصَّدَقَةُ بُرْهَانٌ، وَالصَّبْرُ ضِيَاءٌ، وَالْقُرْآنُ حُجَّةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو، فَبَايِعٌ نَفْسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُهَا»

Kutoka kwa Abu Malik Al-Ash’ariy Mwenyezi Mungu awe radhi naye ambaye amesema:

Mtume rehma na Amani zimshukie amesema: 1- “Usafi ni nusu ya imani, 2- Na kusema: Alhamdulilaah (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) inajaza mizani. 3- Na kusema: Subhaanallah) Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, hujaza au huyajaza yaliyo baina ya mbingu na ardhi. 4- Sala ni Nuru. 5- Na sadaka ni Ushahidi( juu ya Imani). 6- Subira ni mwangaza. 7- Na Qur’ani ni hoja kwako au dhidi yako. 8- Watu wote huondoka asubuhi, kwa hivyo yupo anayeiuza nafsi yake na akaiacha huru na mwengine akaiangamiza.”


Muhtasari wa Maana

Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, anataja baadhi ya milango ya kheri itakayotia uzito zaidi katika mizani ya mja siku ya Qiyaamah, na kwamba mafikio ya watu yamo mikononi mwao, hivyo baadhi yao huokoa nafsi zao na wengine huziangamiza.

Miradi ya Hadithi