108 - MGAWANYIKO WA WATU KATIKA WAHYI (UFUNUO)

عن أبي موسى الأشعريِّ، عن النبيِّ ﷺ قال:«مَثَلُ ما بعَثَني اللهُ به من الهُدى والعِلم، كمَثَل الغَيث الكثيرِ أصاب أرضًا: فكان منها نَقِيَّةٌ، قبِلَت الماءَ، فأنبتَت الكَلَأَ والعُشبَ الكثير، وكانت منها أجادبُ، أمسكت الماءَ، فنفعَ اللهُ بها الناسَ، فشَرِبوا وسَقَوْا وزرعوا، وأصابت منها طائفةٌ أخرى، إنما هي قِيعانٌ لا تُمسِك ماءً ولا تُنبتُ كلأً، فذلك مثَلُ مَن فَقُه في دِين الله، ونفَعه ما بعَثَني الله به فعَلِم وعَلَّم، ومَثلُ مَن لم يرفَعْ بذلك رأسًا، ولم يَقبَلْ هُدى الله الذي أُرسِلْتُ به» متفق عليه.

Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash-Ariyy (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema,

1. Mfano wa aliyonituma kwayo Allah (s.w) miongoni mwa uongofu na elimu, ni kama mfano wa mvua nyingi iliyonyesha katika Ardhi Fulani, 

2. Ikawa Ardhi hiyo ni safi ikapokea maji na kuotesha mazao na mimea. 

3. Na ikawa sehemu nyingine ni kavu ikapokea maji, na Mwenyezi Mungu akawanufaisha watu kwa mvua hiyo wakanywa na wakanywesheleza mifugo na wakalima mazao. 

4. Na ikanyesha sehemu nyingine ya ardhi, hakika sehemuhiyo ni jangwa halihifadhi maji na wala halioteshi mimea  

5. Basi huo ni mfano  wa mtu aliopewa utambuzi katika dini na mwenyezimungu akamnufaisha na yale aliyonitumanayo kwayo, akayatambua na akawaelimisha watu wengine,na mfano wa Yule ambaye  hakuyapa kipaumbele wala hakukubali mwongozo wa mwenyezimungu ambao nimetumwa kwao.(Imepokelewa na Imam Bukhari na Muslimu).

Muhtasari wa Maana

Amefananisha Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake hali za watu katika kupokea mwongozo ambao ameuteremsha Mwenyezi Mungu (s.w) juu ya Mtume wake Muhammad (s.a.w). Katika watu yupo miongoni mwao aliouhifadhi na kuuheshimu, na akafahamu yaliyomo katika mwongozo huo, na akaufanyia kazi, basi akainufaisha nafsi yake na akawa sababu ya kumnufaisha mwengine. Na katika watu kuna mtu anahifadhi elimu kwa ajili ya mtu mwingine zaidi kuliko ufahamu wake mwenyewe, na katika watu kuna watu wameipuuza elimu, wakawa hawakunufaika wenyewe wala hawakuwanufaisha wengine wasiokua wao.

Miradi ya Hadithi