عن ابن عمرَ وأبي هُريرةَ رضي الله عنهم، أنهما سَمعا رسولَ الله يقولُ على أعوادِ مِنْبَرِه: «لَيَنْتَهِيَنَّ أقْوامٌ عن وَدْعِهمُ الجُمُعاتِ، أو لَيَخْتِمَنَّ اللهُ على قُلوبِهم، ثم لَيَكونُنَّ منَ الغافِلينَ»

Kutoka kwa Ibn Umar na Abu Hurayrah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kwamba walimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie akisema akiwa juu ya mimbari yake:

“Watu wakome kuacha Swalah ya Ijumaa. Au Mwenyezi Mungu atawapiga muhuri katika nyoyo zao, kisha wawe miongoni mwa walioghafilika”

Abd al-Rahman bin Sakhr al-Dawsi, al-Azdi, al-Yamani

Abd al-Rahman bin Sakhr al-Dawsi, al-Azdi, al-Yamani, maarufu kwa lakabu yake, na hili jina ndio maarufu zaidi kuliko yote yaliyosemwa kuhusu jina lake na jina la baba yake. Alisilimu katika mwaka wa vita vya Khaybar, na akavishuhudia pamoja na Mtume rehma na Amani zimshukie, kisha akashikamana naye na akadumu humo, Kwa kutaka elimu, mmoja wa masahaba waliohifadhi sana, alikuwa mtawala wa Bahrain kwa kipindi cha ukhalifa wa Omar Ibn Al-Khattab, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kisha akauacha utawala. Alifariki Madina katika mwaka wa (58 AH) [1]

Marejeo

1.  Tazama: “Siyar A’lam al-Nubala” cha al-Dhahabi (4/322), “Al-Tabaqat al-Kubra” cha Ibn Sa’d (4/105), “Al-Isaba fi Tamayez al-Sahaba” na Ibn Hajar (4/155).


Miradi ya Hadithi