عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ، قَالَ: «اجْتَنِبُوا السَّبْعَ المُوبِقَاتِ» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا هُنَّ؟ قَالَ: وَالسِّحْرُ، وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالحَقِّ، وَأَكْلُ الرِّبَا، وَأَكْلُ مَالِ اليَتِيمِ، وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ، وَقَذْفُ المُحْصَنَاتِ المُؤْمِنَاتِ الغَافِلاَتِ». 

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ambaye amesema: 1- “Jiepusheni na madhambi saba yenye kuangamiza.” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni yapi? Akasema Mtume: 2- “Kumshirikisha Mwenyezi Mungu, 3- Na uchawi, 4- Kuiua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu, isipokuwa kwa uadilifu. 5- Kula riba 6- Kula pesa za yatima 7- Kuikimbia vita 8- Na kuwatuhumu na machafu wanawake walio safi, Waumini walioghafilika”

Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anatahadharisha juu ya madhambi makubwa hatari kwa waja, ambayo ni: Shirki, uchawi, kuua pasina haki, riba, pesa ya mayatima, kukimbia vita, na kuwatukana wanawake walio safi

Miradi ya Hadithi