عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ، قَالَ: «اجْتَنِبُوا السَّبْعَ المُوبِقَاتِ» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا هُنَّ؟ قَالَ: وَالسِّحْرُ، وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالحَقِّ، وَأَكْلُ الرِّبَا، وَأَكْلُ مَالِ اليَتِيمِ، وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ، وَقَذْفُ المُحْصَنَاتِ المُؤْمِنَاتِ الغَافِلاَتِ». 

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ambaye amesema: 1- “Jiepusheni na madhambi saba yenye kuangamiza.” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni yapi? Akasema Mtume: 2- “Kumshirikisha Mwenyezi Mungu, 3- Na uchawi, 4- Kuiua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu, isipokuwa kwa uadilifu. 5- Kula riba 6- Kula pesa za yatima 7- Kuikimbia vita 8- Na kuwatuhumu na machafu wanawake walio safi, Waumini walioghafilika”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu: “Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotovu wa mbali”

[An-Nisaai: 116].

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika mji wa Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua”.

[Al-Baqara: 102]

Pia amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa”.

[An-Nisaai: 93]

Na akasema: “Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini (278) Basi ikiwa hamkufanya hivyo jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.”.

[Al-Baqara: 278,279]

Kisha amesema Allah aliyetukuka: “Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhulma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto, na wataingia Motoni” .

[An-Nisaai: 10]

Na amesema Allah utkufufu ni wake: “Enyi Mlio amini! Mkikutana na walio kufuru vitani msiwageuzie mgongo” (15) Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu”

[Al-Anfal: 15, 16]

Na Mwenyezi Mtukufu akasemaa: “Hakika wanao wasingizia wanawake, wanao jihishimu, walio ghafilika, Waumini, wamelaaniwa duniani na Akhera, nao watapata adhabu kubwa”

[An-Nur: 23]



Miradi ya Hadithi