عنْ أَبي سَعيدٍ وأَبي هُرَيْرة - رضيَ اللَّه عَنْهُمَا - عن النَّبيِّ ﷺ قَالَ: «مَا يُصِيبُ الْمُسْلِمَ مِنْ نَصَبٍ وَلا وَصَبٍ وَلا هَمٍّ وَلا حَزَنٍ وَلا أَذًى وَلا غمٍّ، حتَّى الشَّوْكَةُ يُشَاكُها، إِلَّا كفَّر اللَّه بهَا مِنْ خطَايَاه»

Kutoka kwa Abu Said na Abu Hurara – Mwenyezi Mungu awe radhi nao – kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema: “Haimpati mwislamu uchovu, wala maradhi, wasiwasi, huzuni, maumivu, au dhiki. inayompata Mwislamu. Hata kuchomwa kwake na mwiba, ispokuwa Mwenyezi Mungu atamfutia baadhi ya dhambi zake kwa ajili yake.”
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri (155) Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea (156) Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka” .
[Al-Baqara: 155-157]