عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا زَوْجِ النَّبِيِّ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ كَانَ عِنْدَهَا، وَأَنَّهَا سَمِعَتْ صَوْتَ رَجُلٍ يَسْتَأْذِنُ فِي بَيْتِ حَفْصَةَ، قَالَتْ: فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَذَا رَجُلٌ يَسْتَأْذِنُ فِي بَيْتِكَ، فَقَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «أُرَاهُ فُلاَنًا»، لِعَمِّ حَفْصَةَ مِنَ الرَّضَاعَةِ، قَالَتْ عَائِشَةُ: لَوْ كَانَ فُلانٌ حَيًّا - لِعَمِّهَا مِنَ الرَّضَاعَةِ - دَخَلَ عَلَيَّ؟ فَقَالَ: «نَعَمْ؛ الرَّضَاعَةُ تُحَرِّمُ مَا تُحَرِّمُ الوِلادَةُ» 

Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, mke wa Mtume, rehma na amani zimshukie:

1-    Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam alikuwa kwa Aisha, na Aisha akasikia sauti ya mtu akibisha hodi katika nyumba ya Hafsa, : Akasema: Huyu mtu anabisha hodi nyumbani kwako, basi Mtume rehma na amani zimshukie akasema: “Ninamuona ni mtu Fulani ” kwa ami yake Hafsa kwa kunyonya sehemu moja. 2. Aisha akasema: unasemaje lau fulani angekuwa hai - ami yake kwa kunyonya – akaja nyumbani kwangu? Naye akasema: Ndiyo. Kunyonyesha kunayaharamisha yote yaliyoharamishwa kutokana na nasaba na kuzaa”


Muhtasari wa Maana

Mama wa Waumini Aisha Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alimsikia mtu mmoja akiomba ruhusa ya kuingia nyumbani kwa Hafsa, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: “Nadhani ni Fulani.” Akamwambia kwamba kunyonyesha kunakataza kile kinachokatazwa na kuzaa.

Miradi ya Hadithi