عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رضي الله عنهما، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ، وَتَرَاحُمِهِمْ، وَتَعَاطُفِهِمْ، مَثَلُ الْجَسَدِ، إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ، تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى»

Kutoka kwa Nu’man ibn Bashir Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:

Amesema Mtume rehma na Amani zimfikie: “Mfano wa Waumini, katika mapenzi yao, rehema, na upole, ni kama mwili mmoja  Ikiwa kiungo kimoja kitapata kasoro juu yake, sehemu nyingine yote ya mwili inakabiliwa maumivu na kukesha na homa

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Mwenyezi Mungu amesema:

” Enyi mlio amini! Atakaye iacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anaowapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri” .

[Al-Ma’idah: 54]

Amesema Mwenyezi mtukufu:

“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi” .

[At-Tawbah: 71]

Amesema jina lake litukuzwe:

“Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao”

[Al-Fthu: 29]

Miradi ya Hadithi