عن أبي سعيدٍ الخُدريِّ رضي الله عنه، أن النبيَّ ﷺ قال:«لتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ مَن قَبْلَكم، شِبرًا بشِبرٍ، وذراعًا بذراعٍ، حتى لو سَلَكوا جُحْرَ ضَبٍّ لَسَلكْتموه»، قلنا: يا رسول الله، اليهود والنصارى؟ قال: «فمَن؟!»

Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

kwamba Mtume Rehma na Amani zimshukie amesema: 1- “Mtafuata njia za waliotangulia kabla yenu. 2- hatua kwa hatua, dhiraa kwa dhiraa, 3- Hata kama wangeingia kwenye shimo la mburukenge, nanyi mngaliingia.” 4- Tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni Mayahudi na Wakristo? Akasema Mtume Rehma na Amani zimshukie: "basi ni nani kama sio hao?! 

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Tuongoe njia iliyonyooka (6) Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea”

[Al-Fatihah: 6, 7]

Akasema tena umetukuka utukufu wake:

“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu”

[Al-Hadid: 16]

Miradi ya Hadithi