عَنْ مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ «إنَّ أخْوَفَ ما أخافُ عليكم الشِّركُ الأصْغَرُ»، قالوا: وما الشِّركُ الأصْغَرُ يا رسولَ اللهِ؟ قال: «الرِّياءُ؛ يقولُ اللهُ - عزَّ وجلَّ - لهم يومَ القِيامةِ إذا جُزِيَ الناسُ بأعمالِهم: اذْهَبوا إلى الذين كنتُم تُراؤون في الدُّنيا، فانظُروا هل تَجِدون عِندَهُم جزاءً؟!»

Kutoka kwa Mahmood bin Labiid amesema:

amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake): 1. “Hakika ninalo ogopea kwenu zaidi ni shirki ndogo” 2. Wakasema: shirki ndogo ni nini eh Mtume wa Mwenyezi Mungu? 3. Akasema: ni riya yaani kufanya kwa kujionesha 4. Mwenyezi Mungu Mtukufu atawambia siku ya kiyama baada ya watu kulipwa kwa matendo yao: 5. “Nendeni kwa mlio kuwa mnajionesha kwao, muone je watakulipeni?!”


1. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anabainisha na kutahadharisha juu ya jambo hatari lenye kubatilisha ibada, ameliita ushirkina mdogo, ili kutofautisha kati yake na shirki kubwa inayo mtoa mtu katika Uislamu.

2. Wakamuuliza kuhusu ushirikina mdogo; kwa sababu ushirikina unajulikana, nao ni kumuwekea Mwenyezi Mungu mshirika katika mambo ambayo hakuna anaye stahiki zaidi yake. Kutofautisha kati ya ushirikina mdogo na mkubwa inahitaji ufafanuzi zaidi au mfano ili kuweka wazi zaidi.

3. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) akawaeleza kwa mfano ili kuwaweka wazi zaidi, na kwamba jambo analo lihofia zaidi kwenu nyinyi ni riyaa; maana yake ni mtu kudhihirisha ibada kwa watu wafahamu, ili wamtaje vizuri na kumsifia. Huu ndio mfano wa ushirikina mdogo, na mifano mingine ni kuapa kinyume na Mwenyezi Mungu, mtu kusema: ametaka Mwenyezi Mungu na fulani, kuitakidi mikosi, ruqya zisizo kuwa nzuri na mengineyo yasiyo ondoa asili ya Tawhiid kwa kwenda kinyume kabisa, japo kuwa ni aina ya ushirikina [1].

Ijulikane kwamba mambo haya yanaweza kupelekea katika ushirikina mkubwa, kwa sababu mtu anapo apa kinyume na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuitakidi kuwa ni kitukufu, au akimkubali kuhani kwa kudai kwamba anajua ghaibu, na riya ikiwa katika ibada zake zote, au ipo katika kiini cha itikadi yake, au akidhani kwamba hirizi na ruqya ndio vinazuia madhara na kuondoa maradhi, haya yote ni katika ushirikina mkubwa [2] .

4. Kisha Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) akasema kwamba, Mwenyezi Mungu atawaadhibu siku ya kiyama baada ya kuwalipa viumbe, wao wakiwa wanasubiri malipo ya ibada walizo zifanya kwa riya.

5.Mwenyezi Mungu atawambia; nendeni kwa mlio kuwa mnafanya ibada mbele yao ili wawaone na kuwasikia, muone, je mnapata malipo ya ibada zenu? Na hii ni kuwadhihaki na kuwadhalilisha. Mwenyezi Mungu Mtukufu atabatilisha matendo yao mema

amesema Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake):

“amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mimi nimetosheka na washirikina kwa ushirikina wao, yeyote atakae fanya ibada akanishirikisha na chochote, ninamuacha na ushirikina wake”[3].

Lengo analolifikia anae fanya ili watu wamuone, ni kupata sifa kidogo, kisha inafuatia fedheha

amesema Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake):

“mwenye kufanya ibada ili asikike, Mwenyezi Mungu atamfanya asikike, na mwenye kufanya ibada ili aonekane, Mwenyezi Mungu atamfanya aonekane”[4].

Yaani mwenye kukusudia katika ibada yake watu, Mwenyezi Mungu atawafanya waione na kuisikia. Na hayo ndio yatakuwa malipo yake, na huenda Mwenyezi Mungu Mtukufu akamdhalilisha na akadhirishia watu maovu yake asiyo penda yajulikane [5] Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ameeleza kwamba, wakwanza kuchomwa moto siku ya kiyama, ni mtoa sadaka, msoma Qur`ani na anaye ipambania Dini, sababu walifanya hayo ili waonekane, matendo yao yakabatilika na wakakosa malipo [6].

MAFUNDISHO

1. Fuata muongozo wa Mtume wako (Rehma na Amani ziwe juu yake) katika kuwafundisha watu. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ametumia usulubu wa kumfanya mtu aogope na akaweka wazi nasaha mwanzo wa maneno yake, alipo sema (Rehma na Amani ziwe juu yake): “Hakika ninalo ogopea kwenu zaidi”. Ufikishaji wa namna huu unamfanya mtu awe makini na kuhudhurisha akili na usikivu wake, ni bora zaidi kwa anaye toa nasaha atumie usulubu wa kumtamanisha mtu, na kunfanya awe makini.

2. Ushirikina ulio jificha, unaweza kuharibu moyo bila mtu kujua, kwa sababu ameghafilika, mtu anaweza kuingia katika sala au kumtaja Mwenyezi Mungu, au kusoma Qur`an, au kutoa sadaka au mengineyo, akaona watu, akataka waone ibada yake na wasikie sauti yake, kama akipambana na nafsi yake na kuliondosha moyoni kadri awezavyo, halita athiri ibada yake, ama akiendekeza na akabadili niya yake kwenda kwenye riya, ibada hiyo itabatilika. Jifuatilie mwenyewe, na jizoeshe kuwa na Ikhlaas.

3. Twalhat bun Muswarrif -Mwenyezi Mungu amrehemu- alikuwa ni msomaji mzuri wa Qur`ani wa eneo la Kufa, alipo ona kuna watu wengi wanamkubali, aliogopea riya, akaenda kwa A’mash akamsikiliza Qur`ani, watu wakamkubali A’mash na kumuacha Twalhat. Huenda Twalhat [7] alikusudia kuwaonyesha ubora A’mash na wala wasikimbile kwake tu ikampelekea kubadilika, kwani malengo yake ni watu wafaidike.

4. Mja anaweza kudhihirisha ibada, si kwa ajili ya riya, bali anatakata kudhirisha alama za Mwenyezi Mungu, au kuhuisha Sunna iliyo sahaulika,yaani mafundisho ya Mtume, au anafanya ili watu wajifunze kwa vitendo na waathirike, hayo si katika kutaka kujionesha. Riya ni lengo la mtu katika ibada iwe ni watu wamuone ikhalaas, unyenyekevu na ibada yake, na akarizika na hayo.

5. Katika vitu vinavyo weza kusaidia kuondoa riya ni kukumbuka jinsi utakavyo kuwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kumtegemea kiukweli na kumuomba akukinge na riya. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alikuwa akiwatahadharisha maswahaba zake dhidi ya riya, na kuwaamrisha wamuombe Mwenyezi Mungu awakinge.

Kutoka kwa Abuu Musa al Ash’ariy (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yake), amesema:

siku moja Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alituhutubia, akasema: “Enyi watu, ogopeni huu ushirikina, kwa sababu umejificha kuliko vishindo vya sisimizi” mtu mmoja aliye kadiriwa na Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu; tutaiepuka vipi na hali ya kuwa imejificha kuliko kishindo cha sisimizi? Akasema: “semeni: “Eh Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakuomba utuhifadhi tusikushirikishe na chocho tunacho kijua, na tunakuomba msamaha kwa tusicho kijua”[8]

6. Mja anaweza akafanya ibada yoyote kwa ikhlaas, kisha watu wakamuona na kumsifia, akafurahi. Hii haitii dosari ibada yake, na haizingatiwi kuwa ni riya, madamu aliifanya kwa ikhlaas.

Kutoka kwa Abuu Dharri, amesema:

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) aliulizwa: inakuaje mtu akifanya amali njema watu wakamsifia? Akasema: “hiyo ni bishara ya mapema iliyo njema  kwa muumini”[9].

7. Si katika riya mtu kuhamasika kwa kuwepo watu wema, au kuona aibu na kuacha maasi, au akajitahidi kufanya baadhi ya ibada bila kukusudia sifa zao. Hizo ni katika faida za kuwa karibu na watu wema.

8. Mwenye kufanya riya lau angelitizama kwa makini, angeliona kwamba wote anao fanya ili wamuone, hawaoni thamani ya anacho kifanya, wanamsahau baada ya kumaliza, au huenda wakatizama jinsi anavyo fanya riya wakamdharau kwa kuzidisha, au Mwenyezi Mungu kumuazibu kwa fedhea, njia bora ya kuokoka ni kumkusudia Mwenyezi Mungu pekee.

9.Amesema mshairi:

Amepata hasara mwenye kufanya ibada bila kumkusudia Mola wake***anafanya kwa unafiki, hivi kuna unafiki baada ya riya?!

Utapata ulicho tanguliza na kukiwekeza***kama ulivyo fanya, tambua kwamba malipo ni kama ulivyo fanaya.

10.Amesema mwingine:

Eh nafsi usisahau fadhila za Mwenyezi Mungu***kukupa nguvu ni ufalme kwangu na kuniacha ni kuangamia kwangu. Kishindo cha sisimizi juu ya mwamba katika giza***hakijajificha sana kuliko riya na ushirikina



Marejeo

  1. Tazama: “Al-Tawhiyd” cha Ibn Rajab (uk.: 23), “Sherh ya Kashf al-Shubahat, ikifuatiwa na Sharh al-Usul al-Sittah” na Ibn Uthaymiyn (uk.: 115)
  2. .Tazama: “Fath Dhu’l-Jalal wa-Ikram sherh Buloogh Al-Maram” cha Ibn Uthaymiyn (6/357)
  3. .Muslim (2985), kutoka kwa Abu Hurairah
  4. .Muslim (2986), kutoka kwa Ibn Abbas, Mungu amuwiye radhi
  5. .Tazama: “Sharh Sahih Muslim” cha Al-Nawawi (18/116), na linganisha: “Fath Al-Bari” cha Ibn Hajar (11/345)
  6. .Muslim (1905), kutoka kwa Abu Hurairah
  7. ."Sayd al-Khater" cha Ibn al-Jawzi (uk. 292)
  8. .(Ahmad (19109
  9. .Muslim (2642).




Miradi ya Hadithi