عن ابن عبَّاس رضي الله عنه قال: (بُعِثَ رسولُ الله ﷺ لأربعين سنةً، فمكثَ بمكةَ ثلاثَ عشْرةَ سنةً يُوحَى إليه، ثم أُمِر بالهجرةِ فهاجر عشْرَ سنين، ومات وهو ابنُ ثلاثٍ وستينَ سنةً)
عن ابن عبَّاس رضي الله عنه قال: (بُعِثَ رسولُ الله ﷺ لأربعين سنةً، فمكثَ بمكةَ ثلاثَ عشْرةَ سنةً يُوحَى إليه، ثم أُمِر بالهجرةِ فهاجر عشْرَ سنين، ومات وهو ابنُ ثلاثٍ وستينَ سنةً)
kutoka kwa Ibn Abbas (r.a) amesema:“Alipewa utume Nabii Muhammad (s.a.w) Akiwa na umri wa miaka arobaini.Basi alikaa mjini makkat miaka kumi na tatu (13) akipewa ufunuo.Kisha akaamrishwa kuhama basi akahamia Madina miaka kumi.Na alikufa akiwa na umri wa miaka sitini na tatu(63)”
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu
144. " Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? Na atakaye geuka akarudi nyuma huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanao mshukuru ".
[Al Imran: 144].
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia
100. " Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na anaye toka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu ".
[An-Nisa: 100].
Halikadhalika Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema
40. " Ikiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi Mwenyezi Mungu alikwisha mnusuru walipo mtoa walio kufuru, naye ni wa pili katika wawili walipo kuwa katika pango, naye akamwambia sahibu yake: Usihuzunike. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake, na akamuunga mkono kwa majeshi msiyo yaona, na akalifanya neno la walio kufuru kuwa chini, na Neno la Mwenyezi Mungu kuwa ndilo juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima " .
[At-Tawbah: 40].
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia
1. " Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, 2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, 3. Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! 4. Ambaye amefundisha kwa kalamu. 5. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui ".
[Alaq: 1-5]