عن أبي هُرَيرة رضي الله عنه، قال: خطَبَنا رسولُ الله ﷺ، فقال: «أيُّها الناسُ، قد فرَضَ اللهُ عليكم الحجَّ؛ فحُجُّوا»، فقال رجُلٌ: أكلَّ عامٍ يا رسولَ الله؟ فسكَتَ حتى قالها ثلاثًا، فقال رسول الله ﷺ: «لو قلتُ: نَعمْ، لوجَبتْ، ولَمَا استطعتم». ثم قال: «ذَروني ما تركتُكم؛ فإنما هلَك مَن كان قبلَكم بكثرة سؤالهم، واختلافهم على أنبيائهم، فإذا أمرتُكم بشيءٍ فأْتوا منه ما استطعتم، وإذا نَهيتكم عن شيء فدَعوه»


Kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu awe radhi naye ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Amani iwe juu yake alituhutubia na kusema: “Enyi watu, Mwenyezi Mungu amekufaradhisheni Hija; nendeni mkahiji, Akasema mtu mmoja : Je ni kila mwaka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Alinyamaza hadi akasema mara tatu. Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie: “Lau ningesema: Ndio, ingeli kuwa ni wajibu, na msingeliweza. Kisha akasema: Niachieni katika yale ambayo sikukuambieni. Waliangamia walio kuwa kabla yenu kwa sababu ya wingi wa maswali  na kutofautiana kwao na Manabii wao .. Basi nikikuamrisheni kufanya jambo, basi lifanyeni kadiri muwezavyo, na nikikukatazeni, basi liacheni.” 

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Mwenyezi Mungu amesema: “Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu”

[Al-Baqarah: 196]

Na Mwenyezi Mungu amesema “Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu” .

[Al Imran: 97]

Na Mwenyezi Mungu amesema “Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole (101) Waliyauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha wakawa wenye kuyakataa” .

[Al Imran: 97]

Na Mwenyezi Mungu amesema “Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini” .

[Hajj: 78]

Na Mwenyezi Mungu amesema “Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho” .

[Al-Hashr: 7]

Na Mwenyezi Mungu amesema “Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo”

[Al-Taghabun: 16]


Miradi ya Hadithi