3 - KUSUHUDIA KUWA MUHAMMAD NI MTUME WA MWENYEZI MUNGU:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ  قَالَ: «كُلُّ أُمَّتِي يَدْخُلُونَ الجَنَّةَ إِلَّا مَنْ أَبَى»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَنْ يَأْبَى؟ قَالَ: «مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أَبَى» رواه البخاري. 

Kutoka kwa Abu Hurayrah, (Mwenyezi Mungu amuwiye radhi), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani zimshukie) amesema:

1.“Watu wangu wote wataingia Peponi isipokuwa wale wakatao kataa 2.Wakasema Maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani atakayekataa?  3.Akasema Mtume (Rehema na Amani zimshukie): “Mwenye kunitii mimi ataingia Peponi, na mwenye kuniasi atakuwa amekataa.” Imepokewa na Al-Bukhari

  1. Mtume (Rehma na Amani zimfikie) Ameeleza kuwa watu wake wote wataingia Peponi isipokuwa wale watakaokataa, na Makusudio ya kutumia neno Ummah hapa ni Ummah wa kulinganiwa ambao wito wa uislamu umewafikia katika wanadamu na majini, hivyo basi kila mwenye kusikia ulinganizi wa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na akafikiwa na hoja na sheria za Mwenyezi Mungu, basi huyo yumo ndani ya ummah aliotumwa kwao Nabii Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake).

  2. Maswahaba walishangaa kwa hili yaani Vipi mtu mwenye akili timamu atakataa kuingia katika pepo, ambayo kuna neema ambazo jicho halijapata kuziona, wala sikio halijapata kusikia, na moyo wa mwanadamu haujawahi kufikiria? ndio maana waliuliza kwa mshangao kana kwamba wanakanusha mtu kufanya hivyo.

  3. Mtume (Rehma na Amani zimfikie) akawaeleza uhalisia wa jambo hilo, kwamba mwenye kumfuata, na akatekeleza amri zake na akaepuka makatazo yake, huyo atafaulu kuingia peponi na kuwekwa mbali na Moto. Ama mwenye kumuasi na kukiuka amri zake na akatakaa kufuata mwenendo wake, atakuwa amekataa kuingia Peponi mwenyewe kutokana na matendo yake mabaya na imani yake batili.

Na huyu mwenye kukataa mwenyewe kuingia Peponi anaweza kuwa katika walio kufuru, yaani wasiokuwa waislamu kabisa, basi huyu wa aina hii hataingia Peponi milele, kwani Mwenyezi Mungu amesema:

“Na anaye tafuta dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake, na Akhera atakuwa miongoni mwa waliopata khasara.”

[Imran: 85].

Mwenyezi Mungu amesema pia:

“Hakika wale wanao zikanusha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia Peponi mpaka apite ngamia katika tundu ya sindano. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wakosefu”

[Al-A'raf: 40].

Halikadhalika mwenye kukataa kuingia peponi anaweza kuwa miongoni mwa Waislamu waliofuata matamanio na wakaacha maamrisho, na wakafuata njia za waovu, au wakazua katika dini ambayo Mwenyezi Mungu hakuyaridhia, hawa hawataishi Motoni milele; Kwa vile ni Muislamu hatakaa motoni milele, kwani hapa kinachokusudiwa ni kwamba hawataingia Peponi pamoja na waliotangulia (waja wema), bali wataingia peponi baada ya kuhojiwa au kulaumiwa na kuadhibiwa.

Mafunzo

  1. Abu Huraira (Radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesimulia Hadith nyingi kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani zimfikie) hadithi ambazo hakuna mtu mwingine yeyote aliyezisimulia. Kwa sababu ya umakini wake juu ya maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimfikie)   na kujitolea muda wake mwingi kwa ajili ya hilo, kiasi kwamba alikuwa akilala msikitini pamoja na watu waliokuwa wakiishi msikitini, na alikuwa anakula chakula chao na kunywa vinywaji vyao, hashughulishwi na chochote cha kumtoa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, yote hayo ni kutokana na pupa na bidii ya juu zaidi aliyokuwa nayo katika kujifunza dini, kwa hivyo yeyote anayetaka kutafuta elimu au kufika mbali katika jambo fulani basi aige kitendo cha Abu Huraira, subira yake na kushikamana kwake na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimfikie).

  2. Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), katika hadith hii alitoa maneno mafupi yanayohitaji ufafanuzi wa kina zaidi, ili nafsi ziwe tayari kumsikiliza na kukariri atakayoyasema, ndio maana Maswahaba wakawahi kuuliza juu ya ufafanuzi wa jambo hilo. Tunajifunza katika hilo kuwa, Mwalimu, Mlezi, au Mlinganiaji anapaswa kuwa mbunifu katika kutumia mbinu ambazo zitasaidia kuzingatia maneno yake na kuyakariri.

  3. Kuingia Peponi ni ushindi mkubwa unaohitaji kufanyia kazi jambo moja jepesi ambalo ni kumfuata na kumtii Mtume (Rehema na Amani zimshukie).  Atakayeipuuza tunu hiyo hakika atapata hasara, na kupoteza fursa kubwa.

  4. Hakika njia ya kuingia peponi iko wazi na ni nyepesi, haihitaji kuvuka mipaka katika kufanya ibada zisizokuwa na msingi, na uwepesi wake ni kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu Pamoja na Mtume wake, Abdullah bin Masoud anasema: “hakika Sisi tunaiga (mwenendo wa Mtume) na hatuanzishi mapya na tunafuata (maamrisho yake) wala hatuzushi, na hakika hatutapotea maadamu tunashikamana na mafundisho ya Mtume (Rehema na Amani zimshukie)” [1].

  5. Mshairi amesema:Ikiwa wewe si mfuasi wa Muhammad,,,,,,,, basi hujaongoka."Hakika Dunia yako haitakuwa na faida kama hujamfuta yeye ,,,,,,, kwani wewe huwezi kuishi milele?Shida na raha za dunia hii zitaisha,,,,,,,,, = hivyo Basi ipe nyongo achana na starehe za dunia.Kuwa mvumilivu juu katika changamoto zake ,,,,,,, kisha tenda Mema Leo ili kesho ufurahi.

Marejeo

  1. “'Iielam Almuqiein `an Rabi Al a`lamina" Liabn Alqiam” Na Ibn Al-Qayyim (4/115).


Miradi ya Hadithi