عَنْ جَابِرِ بنِ عبدالله - رضي الله عنهما - قَالَ: «لَعَنَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: آكِلَ الرِّبَا، وَمُؤْكِلَهُ، وَكَاتِبَهُ، وَشَاهِدَيْهِ»، وَقَالَ: «هُمْ سَوَاءٌ»

Kutoka kwa Jabir bin Abdullah – Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili – amesema:

1-    “Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, amemlaani 2. mwenye kula riba, mwenye kuilipa, 3. Na Wakala wa riba. 4. Na mwenye kuiandika 5. Na mashahidi wenye kushuhudia riba.” 6. Na akasema Mtume: “Wote wako sawasawa” .

Imepokewa na Muslim (1598).


1- Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anaeleza kutoka kwa Mola wake Mlezi, Mwenye nguvu na Mtukufu: Hakika yeye anawatoa katika rehema yake watu wengi walioshiriki katika uhalifu mmoja.

2-Katika Hadithi hii, Mtume Rehema na Amani zimshukie, amemlaani mwenye kula riba, na ndiye anayechukua pesa kwa watu katika miamala ya riba, sawaawa ikiwa anaitumia kula chakula au matumizi mengine yoyote.

Na riba ni nyongeza ambayo mmoja wa wahusika huchukua kwa kubadilishana pesa kwa pesa bila fidia. Kwa mfano akimkopesha mtu elfu moja kwa sharti ya kuichukua baada ya mwezi, elfu moja na mia mbili, au amemwekea sharti kuwa kucheleweshwa kwa tarehe ya malipo kunaleta faini ya fedha, au anunue bidhaa ya mali ambayo imeandikwa elfu moja na mia mbili kwamba atakusanya tarehe fulani na fulani, halafu mpaka muda unamalizika akajikuta amelipa elfu moja tu. na riba ina aina nyingi sana, na watu huiita katika shughuli za kifedha kwa jina la faida, au faini za kuchelewesha, au majina mengine .

3-Laana pia inamhusu mwenye kuongeza riba, naye ni mhusika aliyekubali kulipa fedha ya ziada kwa kuchelewesha na mengineyo, basi naye amesaidia kula riba, na kwa kawaida riba sio hitaji ambalo maisha ya watu hutegemea, lakini watu wengi huingia katika riba ili kuboresha nyumba au vyombo vya usafiri au vitu vingine.

Na riba inaweza kuwa ongezeko la pesa taslimu, na inaweza kuwa katika kitu kingine. Kama kumpa mtu zawadi na kusema: Nikopeshe elfu; Hata kama akirudisha elfu kamili, hiyo ni riba kwani alizidisha zawadi.

4- Mtume, rehma na amani ziwe juu yake, pia anatuambia kwamba mwandishi anayeandika mkataba wa manunuzi ya riba naye analaaniwa, au kuchangia kuuandika; Iwe ameandika kwa mkono, au kwa mashine, au kwa kubuni hati, au kuingiza data, au kwa njia nyengine.

5- Pia amewalaani mashahidi wawili wanaoshuhudia kuthibitisha haki za wahusika wa riba.

6- Mtume akaeleza kuwa wote ni sawa katika kupata laana, kwa sababu wanashirikiana katika dhambi na uadui, na Mwenyezi Mungu Mtukufu kakataza hayo. Amesema Allah aliye tukuka: “Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui” [Al-Ma’idah: 2].

MAFUNDISHO

1. Sote tunahitaji rehema za Mwenyezi Mungu, na kila mmoja wetu anamuomba Mwenyezi Mungu amrehemu, hivyo kila unaposikia kitu ambacho Mwenyezi Mungu alikilaani au kumlaani mwenye nacho, kikimbie.

2. Huenda baadhi ya watu wakachukizwa na qadar, au ikawaumiza zaidi na kukasirika kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuchelewa kujibu dua yake, na ananong'ona nafsini mwake kwa nini Mungu hakunirehemu? Ingawa anaweza kuwa ameingia katika aina ambazo zinapelekea kulaaniwa na kufukuzwa kutoka kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu, na yeye hajali.

3. Mtu hudanganyika, na huichukulia riba kirahisi, ijapokuwa riba ni miongoni mwa madhambi yenye kuangamiza [1], kwani inaangamiza pesa yake, maisha yake na akhera, basi usiwatii wanaokuita kwenye riba; Iwe ni rafiki mfanyabiashara, au mfumo wa kiuchumi, au kupitia tangazo la kuvutia, Mwenyezi Mungu huondoa baraka kutoka kwa pesa za mlaji riba. Amesema Mwenyezi Mtukufu:

“Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mpingaji na afanyae dhambi”. 

[Al-Baqara: 276]

4. Riba imeharamishwa, na kila mwenye kuishiriki analaaniwa. Hairuhusiwi kushiriki katika mkataba wa riba, hata kama mkopaji akisema, kwa mfano: “Naweza kurudisha kiasi kwa wakati uliowekwa bila riba” kwa sababu uandishi wenyewe wa mkataba umekatazwa, na Mwenyezi Mungu anamlaani mwandishi wa mikataba ya riba.

5. Hakikisha unachuma pesa halali tu. Kula haramu kunamzuia mja kujibiwa dua. Katika Hadith, Mtume Rehema na Amani zimshukie, alimtaja mtu aliyesafiri kwa muda mrefu, akiwa amechafuka na vumbi, ambaye ananyanyua mikono yake mbinguni: Ewe Mola, Mola, hali ya kuwa chakula chake ni haramu, kinywaji chake ni haramu, nguo yake ni haramu, na alirutubishwa kwa chakula cha haramu; Kwa hivyo anawezaje kujibiwa hilo?!» [2] 

6. Wema waliotangulia, Mwenyezi Mungu awawie radhi, walikuwa na shauku ya kupeana chakula kizuri na kuwaonya watu dhidi ya kula haramu. Wahb bin Al-Ward, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Ukisimama katika nafasi ya nguzo hii, hakuna kitakachokufaa mpaka uone kinachoingia tumboni mwako, halali au haramu”[3]  Imam Ahmad bin Hanbal, Mwenyezi Mungu amrehemu, akaulizwa: Ni yapi hulainisha nyoyo? Kisha akatulia kwa muda wa saa moja, kisha akainua kichwa chake na kusema: “Kula halali.” [4] . 

7. Amesema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Usiku niliopelekwa mbinguni niliwaona watu wawili walionijia, wakanipeleka kwenye nchi takatifu, basi tukasafiri mpaka tukafika kwenye mto wa damu, ambamo mtu alikuwa anaogelea amesimama ndani yake, na hapo kandokando kulikuwa na mtu ambaye pembeni yake kuna mawe. Basi yule mtu aliyopo kandokando ya mto akawa anamuelekea yule aliye ndani ya mto, na kila alipotaka kutoka, yule mtu alioko nje akawa anampiga kwa jiwe mdomoni na kumrudisha pale alipokuwa. Ikawa Kila anapotaka kutoka nje, anampiga kwa jiwe, naye anarudi alivyokuwa. Kwa hivyo nikasema hii ni nini? Akasema: Uliyemuona ndani ya mto ni Mla riba” [5].

8. Ikiwa Mwenyezi Mungu amekataza kitu, anakataza na thamani yake, kusaidiana katika hilo, na kushuhudia bila ya kumkemea anaye tenda dhambi hiyo, basi usichangie kufanyika madhambi hata kusema: Sikufanya.

9. Ikiwa uliwahi kujishughulisha na riba na ukataka kutubia, basi rudisha riba kwa wamiliki wake, wala usichukue chochote isipokuwa haki yako ya halali. Kwani Urejeshaji wa mali iliyochukuliwa kwa njia ya dhulma ni sharti la toba.

10. Iwapo kuna mtu anayejihusisha na riba, basi apewe nasaha na kuitwa kwenye haki, na huenda ikamfaa na akaacha kushughulika nayo kwa kumwelimisha na kumkemea, zikiwemo benki zenye biashara za riba na za Kiislamu, lakini hakuna ubaya kwake kushughulika na kitu kinachoruhusiwa ambacho hakipatikani kwa wengine, au ambacho ni ngumu kupata kutoka kwa wengine. Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, aliamiliana na Mayahudi na akauza na akanunua kutoka kwao, nao ni watu wa riba.

11. Mshairi akasema:

Mali ya halali ndio matokeo bora zaidi = na ndio inafaa zaidi kuwa kitu chenye kubakia. Na jihadhari na mali za haramu, kwani ni balaa inapowasilishwa kwenye mizani.

Marejeo

1. Kwa Hadith: “Jiepusheni na madhambi makubwa saba.” Maswahaba Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni madhambi gani? Akasema: “...na kula riba…” Hadiyth imepokelewa na al-Bukhari (6857) na Muslim (89).

2. Imepokewa na Muslim (1015).

3. "Jami' al-'Ulum wa'l-Hukam" cha Ibn Rajab (1/ 263).

4. Manaqib al-Imamu Ahmad cha Ibn al-Jawzi (uk. 269).

5. Imepokewa na Al-Bukhari (2085).


Miradi ya Hadithi