عن مَعْقِلِ بْنِ يَسَارٍ رضي الله عنه ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ : «الْعِبَادَةُ فِي الْهَرْجِ كَهِجْرَةٍ إِلَيَّ»

Kutoka kwa Ma’qil bin Yasar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema: Mtume rehma na Amani zimshukie amesema: “Kuabudu wakati wa ghasia ni kama kuhama kuja kwangu”  .

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anaonesha fadhila kubwa ya ibada katika wakati wa majaribu. Pale ambapo watu wameshughulishwa na matamanio na starehe, dhambi huwa nyingi na kumwagika damu, basi Mtume, amani iwe juu yake, anasema kwamba ibada katika zama 

hizo ni sawa na malipo ya mhajiri aliyeiacha familia yake, nchi yake na fedha zake. kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumtii Mtume, rehma na Amani ziwe juu yake.

Ibada: “Ni Jina linalojumlisha kila anachokipenda Mwenyezi Mungu na anachoridhishwa nacho, kuanzia maneno na vitendo, vya ndani na vya nje, kama vile sala, zaka, saumu, hija, ukweli wa maneno, utimilifu wa amana, kuwaheshimu wazazi, kuunga undugu, kutimiza ahadi, kuamrisha mema na kukataza maovu, jihadi dhidi ya makafiri na wanafiki, kufanya ihsani kwa jirani, yatima, masikini, msafiri na mtumwa na wanyama na dua, dhikr, kisomo, na mfano wa hayo ni ibada, na vilevile kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kumcha Mwenyezi Mungu, kurejea Kwake, kumwamini, kuzivumilia hukumu zake, kushukuru fadhila zake, kuridhika na hukumu yake, kumtegemea Yeye. kutumainia rehema yake, na khofu ya kuadhibiwa kwake, na [1]mfano wa hayo ni sehemu ya kuMuabudu  Mwenyezi Mungu .
Al-Harj: maana yake ni wingi wa fitna na kuenea kwa mauaji, ni kama maneno ya Mtume Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “ Nyakati zitakaribiana, na matendo yatapungua ,na ubahili utaongezeka, na mauaji  [2] yatakithiri ". Wakauliza Maswahaba: Harij ni nini?Akasema Mtume: "Mauwaji mauwaji", 
Badala yake, ibada wakati huo ilikuwa na athari kubwa hasa. Kwa sababu wakati huo kuna uwezekano mkubwa wa watu kutumbukia katika fitna na kughafilika na yale yanayoruhusiwa na yale yaliyoharamishwa, hivyo mwenye kujitenga na watu kwa ujumla ni sawa na Mhamiaji aliyewaacha watu wake juu ya shirki na ukafiri wao, akatoka nje kama mkimbizi wa dini yake .[3]

Mafunzo

1-   Jishughulishe na utiifu, vinginevyo yatakushughulisha madhambi.

2-    Usidanganywe na wingi wa wale wanaoangamia, na wala usikate tamaa kwa kukosa wale wanao pita katika haki, kwani wafuasi wa kila batili ni wengi.

3- Katika Hadith, kuna ushahidi juu ya kujipamba na kujikita katika utiifu wakati watu wanapokuwa wameghafilika, jambo hili linapendwa na Mwenyezi Mungu, kama lilivyokuwa kundi katika wema walo tangulia ambao walipendelea kuhuisha wakati wa baina ya maghribi na ishaa kwa kusali, na wakasema: Ni saa ya kughafilika; Kwa sababu hii, inapendekezwa kusimama katikati ya usiku, ambao watu wengi hawajali kumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake.[4]

4-   Ibada wakati wa mitihani na wakati wa kughafilika, malipo yake ni sawa na kuhama kutoka mji wa ukafiri kwenda katika mji wa  Uislamu, na hakuna malipo yanayozidi yale ya kuhama,

lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

“Wale walio amini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufuzu” .

[Al-Tauwba: 20]

5-   Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam alijulisha kutokea kwa fitna katika mwisho wa zama, ili Muislamu ajiandae kwa hilo na awe tayari kuharakisha utiifu na kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

6-  Ibada katika wakati wa ghasia ni salama kwa watu, lau si waja watiifu katika wakati wa mitihani, Mwenyezi Mungu Mtukufu angeiangamiza ardhi na waliomo ndani yake. Kuwa mwangalifu na uwe mhimili wa usalama kwa Waislamu.

7-  Mshairi alisema:

Ikiwa sijapata kitu cha kujitolea, basi upweke wangu = ni bora zaidi na la kutamanisha zaidi kuliko kukaa na mtu anayevutia. Na mimi kukaa peke yangu kwa ajili ya ibada = inanipendeza zaidi katika maisha yangu kuliko kukaa na rafiki ninaye mwogopa.

Marejeo

  1. Majmuu’ al-Fatawah cha Ibn Taymiyyah (10/149)
  2. .Imepokewa na Al-Bukhari (6037) na Muslim (157).
  3. Tazama: “Lata’if al-Ma’arif” cha Ibn Rajab (uk. 132), “Fayd al-Qadiir” cha al-Manawi (4/373).
  4. Lataif al-Ma'arif cha Ibn Rajab (uk. 131).



Miradi ya Hadithi