104 - KUAHACHA BAADHI YA HALALI KWA KUOGOPEA KUINGIA KATIKA HARAMU

عن النُّعْمانِ بنِ بَشيرٍ – رضي الله عنهما - قال: سمعتُ رسولَ اللهِ ﷺ يقول - وأَهْوى النُّعمانُ بإصْبَعَيْهِ إلى أُذُنَيْهِ -: «إنَّ الحَلالَ بَيِّنٌ، وإنَّ الحَرامَ بَيِّنٌ، وبَيْنَهُما مُشْتَبِهاتٌ لا يَعْلَمُهُنَّ كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ،  فَمَنِ اتَّقى الشُّبُهاتِ اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وعِرْضِهِ، ومَن وقَعَ في الشُّبُهاتِ وقَعَ في الحَرامِ، كالرَّاعِي يَرْعى حَوْلَ الحِمى، يُوشِكُ أنْ يَرْتَعَ فِيهِ، ألا وإنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمًى، ألا وإنَّ حِمى اللهِ مَحارِمُهُ، ألا وإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً، إذا صَلَحَتْ صَلَحَ الجَسَدُ كُلُّهُ، وإذا فَسَدَتْ فَسَدَ الجَسَدُ كُلُّهُ، ألا وهي القَلْبُ».

Kutoka kwa Nuuman bin Bashir – Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili – amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimshukie) akisema – na al-Nu’man aliashiria kwa  vidole vyake kwenye masikio yake:

1. “Halali iko wazi, na haramu iko wazi. 

2. Na kati ya halali na haramu kuna mkanganyiko ambao si watu wengi wanao ufahamu. 

3. Basi mwenye kujiepusha na mashaka atakuwa ameitakasa dhamira na heshima yake ya kidini. 

4. Na anayeingia katika mashaka huanguka katika haramu kama mchungaji anayechunga wanyama wake pembezoni mwa ngome, inakuwa ni karibu zaidi kulisha katika mazao. 

5. Hakika kila Mfalme ana ngome na ulinzi, na hakika ngome ya Mwenyezi Mungu ni mambo yaliyo haramu. 

6. Hakika ndani ya mwili kuna mnofu wa nyama, ukiwa mzuri mnofu huo, basi mwili wote ni mzuri, na ukiharibika mnofu huo mwili wote umeharibika, sasa mnofu huo ndio moyo”

Muhtasari wa Maana

Mtume Rehma na Amani zimshukie anafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amebainisha yale yanayoruhusiwa na yaliyoharamishwa kwa watu, lakini baadhi ya mambo yanaweza kuwatia shaka watu wengi bila ya kujua. Atakayejiepusha na mambo haya ataihifadhi dini yake, na mwenye kutumbukia katika hayo basi ataingia kwenye haramu.
Kisha akamwambia Mtume Rehma na Amani zimshukie kwamba uzuri wa mwili na uharibifu wake unategemea moyo

Miradi ya Hadithi