عن عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ سَمُرَةَ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «يَا عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ سَمُرَةَ، لاَ تَسْأَلِ الإِمَارَةَ؛ فَإِنَّكَ إِنْ أُوتِيتَهَا عَنْ مَسْأَلَةٍ، وُكِلْتَ إِلَيْهَا، وَإِنْ أُوتِيتَهَا مِنْ غَيْرِ مَسْأَلَةٍ، أُعِنْتَ عَلَيْهَا، وَإِذَا حَلَفْتَ عَلَى يَمِينٍ، فَرَأَيْتَ غَيْرَهَا خَيْرًا مِنْهَا، فَكَفِّرْ عَنْ يَمِينِكَ، وَأْتِ الَّذِي هُوَ خَيْرٌ».

Kutoka kwa Abd al-Rahman bin Samra, amesema: Amesema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: 

1- “Ewe Abd al-Rahman ibn Samra, usigombee kuwa kiongozi. 

2- Ukipewa uongozi kwa kugombea na ukikabidhiwa utatelekezewa. 

3- Na ukipewa bila ya kuomba, utasaidiwa tu. 

4- Na ukiapa kiapo na ukaona bora kuliko hicho basi toa kafara ya kiapo kisha ufanye hilo lililo bora zaidi”  

Muhtasari wa Maana

Kusimamia mambo ya watu ni amana kubwa, na hatari yake ni kubwa, kwa hivyo haifai kwa mtu yeyote kuomba awe mtawala, na ikiwa itamfikia bila ya maombi yake, Mwenyezi Mungu humsaidia. Muislamu asifanye kiapo chake kumzuilia kufanya wema, bali afute kiapo chake na afanye wema.

Miradi ya Hadithi