عن ابن عبَّاس رضي الله عنه قال: (بُعِثَ رسولُ الله لأربعين سنةً، فمكثَ بمكةَ ثلاثَ عشْرةَ سنةً يُوحَى إليه، ثم أُمِر بالهجرةِ فهاجر عشْرَ سنين، ومات وهو ابنُ ثلاثٍ وستينَ سنةً)

kutoka kwa Ibn Abbas (r.a) amesema:“Alipewa utume Nabii Muhammad (s.a.w) Akiwa na umri wa miaka arobaini.Basi alikaa mjini makkat miaka kumi na tatu (13) akipewa ufunuo.Kisha akaamrishwa kuhama basi akahamia Madina miaka kumi.Na alikufa akiwa na umri wa miaka sitini na tatu(63)”

Ni Abuu Al-Abbasi, Abdallah Ibn Abbasi Ibn Abdul Al-Muttalib

Ni Abuu Al-Abbasi, Abdallah Ibn Abbasi Ibn Abdul Al-Muttalib, Al-Qurashiy, Al-Hashimiy, Al-Madaniy, alizaliwa kwenye shi’bi ya banii hashim kabla ya kuhama Mtume (s.a.w) kwenda madina kwa miaka mitatu, nayeye (r.a) ndio wino (yaani mwanazuoni mkubwa)  wa ummat Muhammad(s.a.w) na mkalimani wa qur’ani, na mtoto wa ammiyake Mtume (s.a.w), na alikuwa akiitwa bahari kwa wingi wa elimu aliyokuwa nayo, hakika Mtume alimwombea dua kwa kusema: “ Ewe Mwenyezi Mungu mpe ufahamu katika dini ” ([1]) na yeye ni katika maswahaba waliopokea hadithi kwa wingi sana, aliingia katika uislamu akiwa mdogo, na aliishi na Mtume (s.a.w), baada ya

Marejeo

1. Sahihi Al-Bukhari (143) nani tamko lake, na Sahihi Muslim (2477).

Miradi ya Hadithi