عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رضي الله عنهما، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ، وَتَرَاحُمِهِمْ، وَتَعَاطُفِهِمْ، مَثَلُ الْجَسَدِ، إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ، تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى»

Kutoka kwa Nu’man ibn Bashir Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:

Amesema Mtume rehma na Amani zimfikie: “Mfano wa Waumini, katika mapenzi yao, rehema, na upole, ni kama mwili mmoja  Ikiwa kiungo kimoja kitapata kasoro juu yake, sehemu nyingine yote ya mwili inakabiliwa maumivu na kukesha na homa

Muhtasari wa Maana

Mfano wa Waumini katika mapenzi, wema, upendo na huruma wao kwa wao, na mawasiliano na ushirikiano wao, ni kama mfano wa mwili mmoja, ikiwa kiungo kimoja kinauma, kinaathiri viungo vilivyobaki, na matokeo yake ni maumivu, kukosa usingizi na joto la mwili kuongezeka.

Miradi ya Hadithi