39 - KUMUABUDU MWENYEZI MUNGU KATIKA UPENDO NA CHUKI, NA KUPENDA NA KUCHUKIA KWA AJILI YAKE

عَن أَنَسٍ رضي الله عنه، عن النَّبيِّ قال:«ثَلاثٌ مَن كُنَّ فيه وجَدَ حَلاوةَ الإِيمانِ:أَنْ يكونَ اللهُ ورَسُولُه أحَبَّ إلَيهِ ممَّا سِواهُما،وأَنْ يُحِبَّ المَرْءَ لا يُحِبُّه إلا للهِ، وأَنْ يَكْرَهَ أنْ يَعودَ في الكُفْرِ كما يَكْرَهُ أنْ يُقْذَفَ في النَّارِ»

Kutoka kwa Anasi (r.a), kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema:

1. “Mambo matatu yakiwepo kwa mtu atapata ladha ya imani. 2.Ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake ndio wanapendeza kwake zaidi kuliko wasiokuwa hao 3.Na kumpenda mtu na asimpende isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. 4. Na achukie kurudi kwenye ukafiri kama anavyo chukia kutupwa motoni”.



Muhtasari wa Maana

Ameelezea Mtume Muhammad (s.a.w) kunako sifa tatu akizipata mwana Adamu katika nafsi yake hakika atakua ameonja ladha ya imani nazo ni: Awe Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake ndio wanapendeza kwake kuliko kila kitu, na apende kwa ajili ya Mwenyezi Mungu sio kwa ajili ya cheo au maslahi fulani, na iwe kitu anacho kichukia zaidi ni kurudi kwenye ukafiri, kama anavyo chukia kuingia motoni, hivyohivyo ndio auchukie ukafiri na kila kinacho pelekea ukafiri.

Miradi ya Hadithi