عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «حُفَّتِ الْجَنَّةُ بِالْمَكَارِهِ، وَحُفَّتِ النَّارُ بِالشَّهَوَاتِ».

وفي رواية: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ: «حُجِبَتِ النَّارُ بِالشَّهَوَاتِ، وَحُجِبَتِ الجَنَّةُ بِالْمَكَارِهِ»

Kutoka kwa Anas bin Malik, ambaye amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie.

1. “Pepo imezungukwa na yanayo chukiza. 

2. Moto umezungukwa na matamanio”.

Muhtasari wa Maana

Mtume swallallahu alayhi wa sallam, ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka pembezoni mwa Pepo mambo ambayo mtu anayachukia, kama vile majukumu ya kimaamrisho na mengineyo, na akaweka pembezoni mwa Jahannamu mambo ambayo mtu anayatamani kama vile raha na matamanio. Ili mtihani uwe mkubwa zaidi. 

Miradi ya Hadithi