عن عائشةَ رضيَ اللهُ عنها قالت: قالَ رسولُ اللهِ : «مَن أحدَثَ في أمْرِنا هذا ما ليس فيه، فهو رَدٌّ»

Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie: “Mwenye kuzua katika jambo letu hili lisilokuwa ndani yake, litakataliwa.”



Muhtasari wa Maana

Mtume rehma na Amani zimshukie anafahamisha kuwa kufuata ni sharti la kukubaliwa ibada, basi mwenye kuzua kitu katika dini ya Mwenyezi Mungu, kitakataliwa na kurudishwa kwa mwenye nacho, na wala hatalipwa, bali ni mwenye dhambi na mzushi.

Miradi ya Hadithi