عن عائشةَ رضيَ اللهُ عنها قالت: قالَ رسولُ اللهِ : «مَن أحدَثَ في أمْرِنا هذا ما ليس فيه، فهو رَدٌّ»

Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie: “Mwenye kuzua katika jambo letu hili lisilokuwa ndani yake, litakataliwa.”



Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mtukufu:

“Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu”

[Al-An’am: 153].

Mwenyezi mungu amesema:

 “Hakika walio igawa Dini yao na wakawa makundi makundi, huna uhusiano nao wowote. Bila ya shaka jambo lao liko kwa Mwenyezi Mungu; kisha atawaambia yale waliyo kuwa wakiyatenda “.

[Al-An’am: 159]

Na amesema Mwenyezi Mtukufu:

“. Sema ewe Muhammad uwaambie: je, Mwenyezi Mungu amekuruhusuni kufanya hivyo, au mnamzushia Mwenyezi Mungu uongo” .

[Yunus: 59]

Na Amesema Allah Mtukufu:

 “Au hao wana miungu ya kishirikina walio watungia dini asiyokuwa aliyoitolea idhini Mwenyezi Mungu? Na lau lisingekuwako neno la kupambanua basi wangelikatiwa hukumu baina yao. Na hakika wenye kudhulumu watapata adhabu chungu”.

[Al-Shura: 21]

Miradi ya Hadithi