عَنِ الْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ يَقُولُ: «ذَاقَ طَعْمَ الْإِيمَانِ: مَنْ رَضِيَ بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا»

Kutoka kwa al-Abbas ibn Abd al-Muttalib

(Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) kwamba alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani zimshukie) akisema: 1.“Ameipata ladha ya imani. 2. Aliyemridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndio mola wake mlezi  3. Na Uislamu kuwa Dini aliyoichagua. 4. Na Muhammad kuwa ndio Mtume wa haki”

Abu al-Fadhli al-Abbas bin Abd al-Muttalib

Ni: Abu al-Fadhli Mwenyezi Mungu awe Radhi naye, al-Abbas bin Abd al-Muttalib bin Hashim bin Abd Manaf, al-Qurashi, al-Hashimi, al-Makki, baba mdogo wake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na A mani zimshukie), alizaliwa mwaka wa 51 kabla ya kuhama), na alikuwa mmoja wa waheshimiwa wa Kiquraishi kabla ya Uislamu na Uislamu, pia alikuwa mhusika mkuu katika kuuimarisha Msikiti Mtukufu, alisilimu kabla ya kuhama na akauficha Uislamu wake mpaka akatekwa katika vita ya Badr, ndio akadhihirisha kusilimu kwake.Alifariki mwaka wa (32 Hijiria

Miradi ya Hadithi