عن معاويةَ، قال: قال رسول الله ﷺ: «مَن يُرِدِ اللهُ به خيرًا يُفَقِّهْهُ في الدِّينِ، وإنَّما أنا قاسمٌ، واللهُ يُعطِي، ولن تزالَ هذه الأُمَّة قائمةً على أمر الله، لا يَضرُّهم مَن خالَفَهم، حتى يأتيَ أمرُ الله».

Kutoka kwa muawiyah (r.a) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake:

1. “Mwenyezi Mungu anapomtakia kheri mja humpa ufahamu katika dini 

2. Na hakika si vinginevyo, mimi ni mgawaji, na Mwenyezi Mungu ndio anaetoa 

3. Na hautoacha kuendelea huu ummati Muhammad (s.a.w) ukisimama juu ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu, hawawadhuru watakao kwenda kinyume nao, mpaka itakuja amri ya Mwenyezi Mungu” .

Muawuyah Ibn Abiy Suf-Yan

Yeye ni Muawuyah Ibn Abiy Suf-Yan Swakhru Ibn Harbi, Na Mama Yake Ni Hindu Bint Utbat, alisilimu katika umrat ya qadhwaa(iliyokuwa ya kulipa umra iliyopita) na akadhihirisha uislamu wake siku ya kuufungua mji mtukufu wa makkat wakati aliposilimu baba yake, na dada yake ni mama habibat mke wa Mtume muhammad (s.a.w), alikua ni katika waandishi wa ufunuo (wahyi) kwa niaba ya Mtume (s.a.w), na alimtawalisha umaru ibn al-khattab mji wa sham, alichukua mamlaka ya uongozi (khilafa) baada ya fitnat maarufu, na Hussein (r.a) alimu-unga mkono wa ukhalifa, alikufa mwaka (60h) (1)

Marejeo

  1. 1 Tafsiri yake imehakikiwa katika: “Maari-fa fi al-Sahaba cha Abu Naim” (5/2496), “aliastieab fi maarifat al’ashab libn Abd al-Bar” (3/1416), “Asad al-Ghaba cha Ibn al- Athiri” (4/433).


Miradi ya Hadithi