عن معاويةَ، قال: قال رسول الله ﷺ: «مَن يُرِدِ اللهُ به خيرًا يُفَقِّهْهُ في الدِّينِ، وإنَّما أنا قاسمٌ، واللهُ يُعطِي، ولن تزالَ هذه الأُمَّة قائمةً على أمر الله، لا يَضرُّهم مَن خالَفَهم، حتى يأتيَ أمرُ الله».

Kutoka kwa muawiyah (r.a) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake:

1. “Mwenyezi Mungu anapomtakia kheri mja humpa ufahamu katika dini 

2. Na hakika si vinginevyo, mimi ni mgawaji, na Mwenyezi Mungu ndio anaetoa 

3. Na hautoacha kuendelea huu ummati Muhammad (s.a.w) ukisimama juu ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu, hawawadhuru watakao kwenda kinyume nao, mpaka itakuja amri ya Mwenyezi Mungu” .

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Enyi Watu wa Kitabu! Msipetuke mipaka katika dini yenu, wala msimsemee Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha

{An-Nisaa :171 }

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia

 Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakao ulinda

{Al-Hijr : 9}

Halikadhalika Mwenyezi Mungu mtukufu amesema

 Hakika Mwenyezi Mungu huwahami walio amini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila khaini mwingi wa kukanya mema.

{Hajj 38}

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia

 Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi...Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili ".

{Az-Zumar: 9}

Halikadhalika Mwenyezi Mungu mtukufu amesema

Je! Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfungulia kifua chake kwa Uislamu, na akawa yuko kwenye nuru itokayo kwa Mola wake Mlezi (ni sawa na mwenye moyo mgumu?) Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisio mkumbuka Mwenyezi Mungu! Hao wamo katika upotofu wa dhaahiri. Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa ".

{ Az-Zumar 22- 23}

Miradi ya Hadithi