عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ اللهُ فِي ظِلِّهِ يَوْمَ لَا ظِلَّ إلَّا ظِلُّهُ: الْإِمَامُ الْعَادِلُ، وَشَابٌّ نَشَأَ بِعِبَادَةِ اللهِ عز وجل، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ فِي الْمَسَاجِدِ، وَرَجُلَانِ تَحَابَّا فِي اللهِ؛ اجْتَمَعَا عَلَيْهِ، وَتَفَرَّقَا عَلَيْهِ، وَرَجُلٌ دَعَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ وَجَمَالٍ، فَقَالَ: إِنِّي أَخَافُ اللهَ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ، فَأَخْفَاهَا حَتَّى لَا تَعْلَمَ يَمِينُهُ مَا تُنْفِقُ شِمَالُهُ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ اللهَ خَالِيًا فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ.

Kwa kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema: 1- “Watu aina saba Mwenyezi Mungu atawatia kwenye kivuli chake siku ambayo hakuna kivuli ila chake. 2- Imamu Muadilifu 3- Kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu. 4- Mtu ambaye moyo wake umefungamana na misikiti. 5- Watu wawili waliopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. wakakusanyika kwa ajili yake na kutawanyika kwa ajili yake. 6- Mwanaume aliyekaribishwa na mwanamke mwenye cheo na mrembo, akasema: Mimi namuogopa Mwenyezi Mungu. 7- Mtu aliyetoa sadaka na akaificha mpaka mkono wake wa kushoto usijue mkono wake wa kulia unatoa nini. 8- Na mtu aliye mtaja Mwenyezi Mungu kwa siri, mpaka akalia”.


Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anataja makundi ya Waislamu ambao Mwenyezi Mungu atawatia kwenye kivuli chake Siku ya Kiyama, na watakuwa salama na joto la jua na uvundo wa Jahannam. Nao ni: Imamu muadilifu, kijana mtiifu kwa Allah, mwenye kushikamana na misikiti, mwenye kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mwenye kuacha matamanio kwa ajili ya kumcha Mungu, mwenye kuficha sadaka yake, mwenye kulia katika upweke wake kwa kumcha Mungu.

Miradi ya Hadithi