عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بن مسعود ، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «عَلَيْكُمْ بِالصِّدْقِ، فَإِنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى الْبِرِّ، وَإِنَّ الْبِرَّ يَهْدِي إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَصْدُقُ وَيَتَحَرَّى الصِّدْقَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ صِدِّيقًا، وَإِيَّاكُمْ وَالْكَذِبَ، فَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ، وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَكْذِبُ وَيَتَحَرَّى الْكَذِبَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ كَذَّابًا».

Kutoka kwa Abdullah bin Masoud Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka kwa Mtume, rehma na Amani zimshukie, ambaye amesema:

1- “kuweni wakweli, kwani ukweli humpeleka mtu kwenye wema, na wema humwongoza mtu kwenye Pepo, Na mtu huendelea kusema ukweli na kujitahidi kuwa mkweli mpaka aandikishwe kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli.  

2- Na mwache kusema uongo, kwani uongo humpeleka mtu kwenye uovu, na uovu humwongoza mtu kwenye moto, na mtu huendelea kusema uongo na kujitahidi katika uongo mpaka, anaandikwa kwa Mwenyezi mungu kuwa ni mwongo.

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

“Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: “Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wako pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Wasemao kweli, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!”.

[An-Nisa: 69]

“Na akasema pia: “Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli” .

[At-Tawba: 119]

“Akasema pia: “Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema. (13) Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni” .

[Al-Infitar: 13, 14]

Miradi ya Hadithi