عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بن مسعود ، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «عَلَيْكُمْ بِالصِّدْقِ، فَإِنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى الْبِرِّ، وَإِنَّ الْبِرَّ يَهْدِي إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَصْدُقُ وَيَتَحَرَّى الصِّدْقَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ صِدِّيقًا، وَإِيَّاكُمْ وَالْكَذِبَ، فَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ، وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَكْذِبُ وَيَتَحَرَّى الْكَذِبَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ كَذَّابًا».

Kutoka kwa Abdullah bin Masoud Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka kwa Mtume, rehma na Amani zimshukie, ambaye amesema:

1- “kuweni wakweli, kwani ukweli humpeleka mtu kwenye wema, na wema humwongoza mtu kwenye Pepo, Na mtu huendelea kusema ukweli na kujitahidi kuwa mkweli mpaka aandikishwe kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli.  

2- Na mwache kusema uongo, kwani uongo humpeleka mtu kwenye uovu, na uovu humwongoza mtu kwenye moto, na mtu huendelea kusema uongo na kujitahidi katika uongo mpaka, anaandikwa kwa Mwenyezi mungu kuwa ni mwongo.


1. Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, anauamrisha umma wake ushikamane na kusema kweli; ukweli unamwongoza mtu kwenye wema, nalo ni jina lililokusanya kila kheri, na hilo linampeleka kuingia Peponi. Na Muislamu ni mkweli na anauzoea ukweli na anadumu nao katika hali ya dhiki na faraja mpaka anaandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli.
Na mtu mkweli: Ni mwenye kudumu katika ukweli ambaye hasemi uongo. Ikiwa mja ametawaliwa na ukweli, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu humwandika kuwa ni mkweli, basi anajulikana miongoni mwa watu kwa ukweli wake ikiwa ni fahari kwake, vile vile hukubalika kwa watu. Na anasifika kwa hilo katika mkusanyiko wa waja wema kabisa ikiwa ni malipo ya ukweli wake, na Mola Mtukufu amemweka katika kundi la wakweli, na hao ndio watu wa daraja la juu baada ya Manabii.” Amesema Mwenyezi Mungu:

“Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Wasemao kweli, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!”

[An-Nisa: 69]


Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaamrisha waja wake kuwa wakweli na waingie katika kundi la wakweli.

” Amesema Yeye Aliyetukuka: “Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli” .

[At-Tawba: 119]

Na Mtume amani iwe juu yake ameeleza kwamba watu bora ni wasemao kweli; Kutoka kwa Abdullah bin Amr bin Al-Aas-radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Aliambiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wasallam: Ni watu gani bora? Akasema Mtume: "Mcha Mungu safi, ambaye ni mkweli wa ulimi"  [1]


2. Mtume, amani iwe juu yake, alionya dhidi ya kusema uwongo. Uongo ndio msingi wa maovu yote, na ndio kiongozi wa ufisadi na uasi, na hilo hupelekea mwongo kutupwa motoni. Na Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alielezea kwamba ikiwa mtu amezoea kusema uwongo, ataandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mwongo, na atajulikana kwa watu kuwa ni mwongo na kumuelezea hivyo na kumlaumu kwa sifa hiyo. Hivyo basi, atafedheheshwa mbele ya watu wa wa juu kabisa, na Siku ya Kiyama atafufuliwa akiwa katika kundi la wanafiki.


Na Mtume akaelezea kwamba uwongo ni miongoni mwa sifa na dalili za wanaafiki, amesema Mtume Rehema na amani zimshukie: “Alama za mnafiki ni tatu. Anapozungumza anasema uwongo, anapotoa ahadi anaivunja, na akikabidhiwa amana anafanya khiyana”  [2]


Na Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam ameweka usafi wa mja na uharibifu wake unatokana na ulimi; Na akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Imani ya mja haiwi safi sana mpaka moyo wake unyooke, na moyo wake hautakuwa sawa na safi mpaka ulimi wake unyooke”  [3]


1. kuwa mkweli; Ni kupambanua kati ya unafiki na imani, na ukweli ndio hukumu ya uadilifu baina ya watu wa Peponi na watu wa Motoni.


2. Ukweli ni daraja ya juu kabisa katika Uislamu, na ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akawausia waja wake kuwa pamoja na wakweli, na akafanya malipo ya wale wanaofanya utiifu wafufuliwe pamoja na wakweli, na hii inaashiria hadhi yao kubwa. na ukaribu wao na Mwenyezi Mungu. Je, hii haitushawishi kuwa na hamu ya kusema kweli?!


3. Mwenyezi Mungu ameutakasa ulimi kuliko viungo vyote, na akainua daraja yake, na akadhihirisha wema wake, kwa kuufanya useme miongoni mwa viungo vyote kwa upweke wake. Si vyema kwa Muislamu kuuzoesha ulimi wake kusema uongo. Bali, ni lazima auzoeshe kudumu katika kusema kweli, na nini kitamnufaisha katika nyumba zake. kwa sababu ulimi hufuata kilicho zoeleka; Ikiwa ni kweli, basi ni kweli, na ikiwa si kweli, basi ni uongo.


4. Ukitaka kuboresha athari zako kwa watu, usiruhusu wakushutumu kwa uwongo au tuhuma, kwa hivyo kuwa mkweli. Mwenyezi Mungu atakuandika miongoni mwa watu wema, na atakufanya ukubalike kwa watu katika ardhi.


5. Kusema kweli hupandisha daraja za mja duniani na Akhera; aliulizwa Luquman Al-Hakim, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi: “Ni ibada zipi zimekufikisha daraja hizi ulizonazo? Akasema: Kusema kweli, utimilifu wa amana, na kuacha yasiyonihusu.  [4]


6. Ukweli ni miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na ni nani mkweli zaidi katika mazungumzo kuliko Mwenyezi Mungu”

[An-Nisa: 87]

 na akasema, vilevile :

“Ni nani mkweli zaidi kuliko Mwenyezi Mungu katika kauli”

[An-Nisa: 122]

. Basi kwa nini tusifanane na Mungu Mwenyezi katika sifa zake!


7. Ukitaka kuwa na vitendo vizuri, basi anza kusafisha maneno, na wala usizungumze ila kweli tupu; ukweli huongoza kwenye wema. Yunus bin Ubaid, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Sijamuona yeyote mwenye ulimi wa kusema kweli, isipokuwa niliona hata matendo yake mengine yanakuwa safi”  [5]


8. Usifikirie kuwa wokovu upo katika kusema uwongo. Huenda hila zako na uwongo wako ukawadanganya watu, lakini hutamdanganya Mola wako Mlezi. Kwa hivyo lazima uwe mkweli utasalimika. Huyu Ka’b bin Malik, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alipoacha kushiriki vita vya Tabuk, na wanafiki wakamjia Mtume, amani ziwe juu yake, wakimwomba msamaha kwa uwongo na ujanja. Alikataa kusema uongo badala yake alimweleza ukweli, na Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam aliyaamini aliyoyasema, na matokeo ya hayo ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliikubali toba yake, na akateremsha Aya juu yake zilizosomwa, na akazikhitimisha kwa kauli yake Allah Mtukufu:

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli”[6]

[At-Tawba: 119]

 
9. Mshairi alisema:
Na ikiwa mambo hayaeleweki = basi ukweli ndio bora zaidi yao.
Ukweli kumfunika kichwani= mhusika wake taji la kusema kweli
Na uaminifu huondosha ubaya ukanda wake = katika kila pande na kutia taa
10. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewatishia waongo adhabu katika Moto, na Mwenyezi Mungu atukinge nayo, akasema:

“Ole wake kila Mwongo wenye dhambi”

[Al-Jathiya: 7]

. Basi jihadhari na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
11. Aina kali zaidi ya uwongo: Ni Kumzulia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kukataza Aliyoyaruhusu na kuruhusu Aliyoharamisha, kumkashifu Mwenyezi Mungu na kusema juu Yake bila ya kujua. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali, na hichi haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa (116) Ni starehe ndogo, nao watapata adhabu chungu”

[An-Nahl: 116, 117]

Basi jihadhari na kusema katika sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu bila ya elimu, sema: Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi, na muongoze muulizaji kwa watu wa elimu na fatwa, kwani hilo ni bora kuliko kutumbukia kwenye batili na kumkashifu Mwenyezi Mungu Mtukufu.


12. Jiepusheni kabisa na kusema uwongo, wala usiongope kwa kukusudia au mzaha.

Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie:

“Ole wake mwenye kusema uwongo ili kuwafanya watu wamchekee, ole wake na ole wake”  [7]


13. Mshairi alisema:
Umesema uwongo, na anayesema uwongo, malipo yake = ikiwa atasema ukweli ni kwamba hataaminiki.
Mwongo akijulikana kuwa ni mwongo bado = ni mwongo mbele ya watu hata akiwa mkweli.
Na katika maafa ya mwongo ni kusahau uwongo wake = na utamwona kama mwerevu akishabobea.

Marejeo

  1. Imepokewa na Ibn Majah (4216).
  2.  Imepokewa na Al-Bukhari (33) na Muslim (59).
  3.  Imepokewa na Ahmad (13079).
  4.  Imepokewa na Abu Naim katika Hilyat al-Awliya’ (6/328).
  5. Imepokewa na Ibn Abi Asim katika Al-Zuhd (112), na Ibn Abi Al-Dunya katika Al-Samt (60).
  6.  Imepokewa na Al-Bukhari (4418) na Muslim (2769).
  7.  Imepokewa na Abu Daawuud (4990) na Al-Tirmidhiy (2315).


Miradi ya Hadithi