عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بن مسعود ، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «عَلَيْكُمْ بِالصِّدْقِ، فَإِنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى الْبِرِّ، وَإِنَّ الْبِرَّ يَهْدِي إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَصْدُقُ وَيَتَحَرَّى الصِّدْقَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ صِدِّيقًا، وَإِيَّاكُمْ وَالْكَذِبَ، فَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ، وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَكْذِبُ وَيَتَحَرَّى الْكَذِبَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ كَذَّابًا».

Kutoka kwa Abdullah bin Masoud Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka kwa Mtume, rehma na Amani zimshukie, ambaye amesema:

1- “kuweni wakweli, kwani ukweli humpeleka mtu kwenye wema, na wema humwongoza mtu kwenye Pepo, Na mtu huendelea kusema ukweli na kujitahidi kuwa mkweli mpaka aandikishwe kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli.  

2- Na mwache kusema uongo, kwani uongo humpeleka mtu kwenye uovu, na uovu humwongoza mtu kwenye moto, na mtu huendelea kusema uongo na kujitahidi katika uongo mpaka, anaandikwa kwa Mwenyezi mungu kuwa ni mwongo.

Abdullah bin Masoud

Ni: Abdullah bin Masoud bin Ghafil bin Habib, Al-Hudhali, Abu Abd al-Rahman, sahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam aliyesilimu huko Makkah zamani, alihama marambili, na alishiriki vita vya Badr na matukio yote pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie na ndiye mbeba viatu vya Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, alikuwa akimvisha Mtume anaposimama, na kuvibeba mikononi mwake anapokaa mtume amani iwe juu yake, alikufa huko Madina katika mwaka wa (32 AH) au (33 AH) [1]

Marejeo

  1. Rejea ufafanuzi wake katika: “Ma’rifat al-Sahaba” na Abu Na’im (4/ 1765), “Al-Istifa’ fi Ma’rifat al-Ashab” cha Ibn Abd al-Barr (3/987). “Al-Isaba fi Tamayez al-Sahaba” cha Ibn Hajar (4/198).


Miradi ya Hadithi