عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رضي الله عنها، أَنَّ رَسُولَ اللهِ  قَالَ: «لَا تُحِدُّ امْرَأَةٌ عَلَى مَيِّتٍ فَوْقَ ثَلَاثٍ، إِلَّا عَلَى زَوْجٍ، أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا، وَلَا تَلْبَسُ ثَوْبًا مَصْبُوغًا، إِلَّا ثَوْبَ عَصْبٍ، وَلَا تَكْتَحِلُ، وَلَا تَمَسُّ طِيبًا، إِلَّا إِذَا طَهُرَتْ، نُبْذَةً مِنْ قُسْطٍ أَوْ أَظْفَارٍ»


Kutoka kwa Ummu Atiyah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume

wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema: 1. “Mwanamke hakai matanga kwa kufa yoyote zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa kufiwa na mume atakaa miezi minne na masiku kumi.  2.Wala havai nguo iliyo tiwa rangirangi isipokuwa nguo pana ya moja kwa moja, na wala asipakae wanja, na wala asiguse manukato na marashi isipokuwa akiwa safi baada ya hedhi. Atumie kiasi kidogo cha marashi na manukato au kucha”


Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam ameeleza kuwa mwanamke haruhusiwi kuomboleza kwa kufa yeyote yule zaidi ya siku tatu isipokuwa mume; Ni miezi minne na siku kumi. Katika kipindi hicho, havai nguo za rangi, wala hatakiwi kupaka wanja, wala manukato, isipokuwa anapotoharika kutokana na hedhi yake, basi hugusa manukato kidogo ili harufu mbaya ya damu imtoweke.

Miradi ya Hadithi