عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رضي الله عنها، أَنَّ رَسُولَ اللهِ  قَالَ: «لَا تُحِدُّ امْرَأَةٌ عَلَى مَيِّتٍ فَوْقَ ثَلَاثٍ، إِلَّا عَلَى زَوْجٍ، أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا، وَلَا تَلْبَسُ ثَوْبًا مَصْبُوغًا، إِلَّا ثَوْبَ عَصْبٍ، وَلَا تَكْتَحِلُ، وَلَا تَمَسُّ طِيبًا، إِلَّا إِذَا طَهُرَتْ، نُبْذَةً مِنْ قُسْطٍ أَوْ أَظْفَارٍ»


Kutoka kwa Ummu Atiyah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume

wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema: 1. “Mwanamke hakai matanga kwa kufa yoyote zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa kufiwa na mume atakaa miezi minne na masiku kumi.  2.Wala havai nguo iliyo tiwa rangirangi isipokuwa nguo pana ya moja kwa moja, na wala asipakae wanja, na wala asiguse manukato na marashi isipokuwa akiwa safi baada ya hedhi. Atumie kiasi kidogo cha marashi na manukato au kucha”


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu

: “Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi mine na siku kumi. Na wanapo timiza eda yao basi hapana ubaya kwenu wanamume kwa wanao jifanyia kwa mujibu wa ada. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda”

[Al-Baqarah: 234]


Miradi ya Hadithi