عن عبدِ الله بنِ مُعاويةَ رضي الله عنه ، قال: قال النبيُّ :«ثلاثٌ مَن فعَلهنَّ فقد طَعِمَ طَعْمَ الإيمانِ:مَن عبَدَ اللهَ وحدَه، وأنه لا إلهَ إلا اللهُ،وأعطى زكاةَ ماله طيِّبةً بها نفْسُهُ، رافدةً عليه كلَّ عام،ولا يُعطي الهَرِمةَ، ولا الدَّرِنةَ، ولا المريضةَ، ولا الشَّرَطَ اللئيمةَ؛ولكنْ مِن وسَطِ أموالكم؛ فإنَّ اللهَ لم يَسألْكم خيرَه، ولم يأمُرْكم بشرِّه»

Kutoka kwa Abdullah bin Muawiyah Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema: Mtume, rehma na Amani zimshukie, amesema:

“Mambo matatu atakaye yafanya ameonja ladha ya imani. Mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba hapana mungu mwingine ila yeye Mwenyezi Mungu. Akatoa zaka ya mali yake kwa niya njema kutoka moyoni mwake, haliyakuwa nafsi yake inamuamuru kufanya hivyo kila mwaka. Hatoi mnyama aliyezeeka, wala mwenye ugonjwa wa ngozi, wala mgonjwa, wala dhaifu; Lakini toeni za kati na kati katika mali zenu; Mwenyezi Mungu hakukuombeni vilivyo bora zaidi, wala hakukuamrisheni mtoe vibaya.”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mungu:

“Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na Watumwa”

[Al-Baqarah: 177]. 

Na Mwenyezi Mungu Amesema:

“Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa”

[Al-Baqarah: 267].

Na Allah aliyetukuka amesema:

“Kabisa Hamtafikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua”

[Al Imran: 92].

Mwenyezi mtukufu amesema pia:

“Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu chochote, Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotovu wa mbali”

[An-Nisa: 116].

Na akasema Allah aliyetukuka:

“Na haikuwazuilia kukubaliwa sadaka zao ila kwa kuwa walimkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaji kwenye Sala ila kwa uvivu, wala hawatoi michango ila katika hali ya  kuchukia”

[At-Tawbah: 54]

Miradi ya Hadithi