عن عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه، قال: كُنَّا مع النبيِّ شَبابًا لا نجدُ شيئًا، فقال لنا رسولُ الله ﷺ: «يا معشرَ الشباب، مَن استطاع الباءةَ، فليتزوَّجْ؛ فإنه أغَضُّ للبصر، وأحصَنُ للفَرْجِ، ومَن لم يستطِعْ، فعليه بالصَّوْمِ؛ فإنه له وِجاءٌ»
عن عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه، قال: كُنَّا مع النبيِّ شَبابًا لا نجدُ شيئًا، فقال لنا رسولُ الله ﷺ: «يا معشرَ الشباب، مَن استطاع الباءةَ، فليتزوَّجْ؛ فإنه أغَضُّ للبصر، وأحصَنُ للفَرْجِ، ومَن لم يستطِعْ، فعليه بالصَّوْمِ؛ فإنه له وِجاءٌ»
Kutoka kwa Abdullah bin Masoud, radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume, ilihali tukiwa vijana, hatuna chochote, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam akatuambia: 1- “Enyi kijana, anayeweza kusimamia majukumu ya ndoa basi na aoe. Ndoa Inapunguza macho na kuimarisha uke. 2- Iwapo mtu hawezi kufanya hivyo ni lazima afunge. Hakika kufunga ni kinga.
Mwenyezi Mungu amesema: “Enyi mlio amini! Mmefaradhishiwa kufunga, kama walivyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuwa wachamungu”
[Al-Baqarah: 183].
Na amesema Mwenyezi Mtukufu: “Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Kufanya hivyo ni kujitakasa zaidi kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za wanayo yafanya (30) Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika” .
[An-Nur: 30, 31]
Pia akasema Mwenyezi Mungu mtukufu: “Na wajizuie na machafu wale wasio pata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe kwa fadhila yake”
[An-Nur: 33].
Pia akasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: “Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri”.
[Al-Rum: 21]