عَنْ عَمْرِو بنِ العَاصِ رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا جَعَلَ اللهُ الْإِسْلامَ فِي قَلْبِي، أَتَيْتُ النَّبِيَّ ﷺ، فَقُلْتُ: ابْسُطْ يَمِينَكَ فَلْأُبَايِعْكَ، فَبَسَطَ يَمِينَهُ، قَالَ: فَقَبَضْتُ يَدِي. قَالَ: «مَا لَكَ يَا عَمْرُو؟» قَالَ: قُلْتُ: أَرَدْتُ أَنْ أَشْتَرِطَ، قَالَ: «تَشْتَرِطُ بِمَاذَا؟» قُلْتُ: أَنْ يُغْفَرَ لِي، قَالَ: «أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ الْإِسْلَامَ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ؟ وَأَنَّ الهِجْرَةَ تَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهَا؟ وَأَنَّ الحَجَّ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ؟»

Kutoka kwa Amr Ibn Al-Aas, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

1- Mwenyezi Mungu alipouweka Uislamu moyoni mwangu, nilimjia Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam na nikasema: “Kunjua mkono wako na nikupe kiapo cha utii. 

2- Kisha akanyoosha mkono wake, na akasema: nikazuwia mkono wangu. Akasema Mtume: “Una nini ewe Amr? Akasema: Nikasema: Nataka kukupa sharti, akasema Mtume: “Unaweka sharti la nini?” Nikasema: kusamehewa, 

3- Akasema Mtume: “Je, hujui kwamba Uislamu unafuta yaliyotangulia? 

4- Na kuhama kunafutilia mbali yaliyokuwa kabla yake? 

5- Na kwamba Hija inafuta yaliyotangulia kabla yake?”

Muhtasari wa Maana

Amr, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, aliogopa kwamba ataadhibiwa kwa yale aliyoyafanya kabla ya kusilimu kwake, hivyo alitaka kuweka masharti kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amsamehe kwa hilo kabla hajasilimu.

Miradi ya Hadithi