عَنْ عَمْرِو بنِ العَاصِ رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا جَعَلَ اللهُ الْإِسْلامَ فِي قَلْبِي، أَتَيْتُ النَّبِيَّ ﷺ، فَقُلْتُ: ابْسُطْ يَمِينَكَ فَلْأُبَايِعْكَ، فَبَسَطَ يَمِينَهُ، قَالَ: فَقَبَضْتُ يَدِي. قَالَ: «مَا لَكَ يَا عَمْرُو؟» قَالَ: قُلْتُ: أَرَدْتُ أَنْ أَشْتَرِطَ، قَالَ: «تَشْتَرِطُ بِمَاذَا؟» قُلْتُ: أَنْ يُغْفَرَ لِي، قَالَ: «أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ الْإِسْلَامَ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ؟ وَأَنَّ الهِجْرَةَ تَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهَا؟ وَأَنَّ الحَجَّ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ؟»

Kutoka kwa Amr Ibn Al-Aas, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

1- Mwenyezi Mungu alipouweka Uislamu moyoni mwangu, nilimjia Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam na nikasema: “Kunjua mkono wako na nikupe kiapo cha utii. 

2- Kisha akanyoosha mkono wake, na akasema: nikazuwia mkono wangu. Akasema Mtume: “Una nini ewe Amr? Akasema: Nikasema: Nataka kukupa sharti, akasema Mtume: “Unaweka sharti la nini?” Nikasema: kusamehewa, 

3- Akasema Mtume: “Je, hujui kwamba Uislamu unafuta yaliyotangulia? 

4- Na kuhama kunafutilia mbali yaliyokuwa kabla yake? 

5- Na kwamba Hija inafuta yaliyotangulia kabla yake?”

Ni: Abu Abdullah, Amr bin Al-Aas bin Wael,

Ni: Abu Abdullah, Amr bin Al-Aas bin Wael, Al- Qurashi, Al-Sahmi, mwerevu wa Makureshi, na ali - yeufungua mji wa Misri. Alipigiwa mfano kwa kuwa na akili, busara na uimara, na yeye ndiye ambaye Maquraishi walimtuma kwa Mfalme Al-Najashiy ili kuwarudishia waislamu waliokuwa kwake mion - goni mwa Waislamu. Alisilimu katika mwaka wa nane wa Hijra, miezi sita kabla ya kufunguliwa Mji tukufu wa Makka, na akahamia kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, alikufa katika mwaka wa (43 AH) [1]

Marejeo

1. Tazama: “Ma’rifat al-Sahaba” cha Abu Naim (4/ 1987), “Al-Is - ti’ab fi Ma’rifat al-Ashab” cha Ibn Abd al-Barr (3/ 1184), “Asad al-Ghaba” cha Ibn al-Athir (3/ 741).


Miradi ya Hadithi