عَنْ وَرَّادٍ، كَاتِبِ المُغِيرَةِ، قَالَ: كَتَبَ مُعَاوِيَةُ إِلَى المُغِيرَةِ رضي الله عنهما: اكْتُبْ إِلَيَّ مَا سَمِعْتَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ ﷺ، فَكَتَبَ إِلَيْهِ: إِنَّ نَبِيَّ اللَّهِ ﷺ كَانَ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاةٍ: «لا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ، وَلَهُ الحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، اللَّهُمَّ لا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ، وَلا يَنْفَعُ ذَا الجَدِّ مِنْكَ الجَدُّ» وَكَتَبَ إِلَيْهِ: إِنَّه: «كَانَ يَنْهَى عَنْ قِيلَ وَقَالَ، وَكَثْرَةِ السُّؤَالِ، وَإِضَاعَةِ المَالِ، وَكَانَ يَنْهَى عَنْ عُقُوقِ الأُمَّهَاتِ، وَوَأْدِ البَنَاتِ، وَمَنْعٍ وَهَاتِ».

Kutoka kwa Warad, Mwandishi wa Al-Mughirah, amesema:Muawiya alimwandikia Al-Mughirah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili:

1- Niandikie uliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie na akamwandikia: 2- Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam alikuwa akisema kila baada ya kila swala: “Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja, Peke Yake, hana mshirika, ufalme ni wake, sifa njema ni zake, na Yeye ni Muweza wa yote. 3- Ewe Mwenyezi Mungu hakuna kizuizi kwa ulichotoa wala mtoaji kwa ulicho kizuia. 4- Na hanufaishi mwenye utukufu, bali utukufu ni wako” 5- Na akamuandikia: “Alikuwa akiharamisha yaliyosemwa na kusengenya. 6- Kuuliza sana 7- Kupoteza pesa 8- Amekataza kuwaasi akina mama. 9- Mauaji ya watoto wachanga wa kike 10- Na kuzuia (kuwa na choyo) na kuchukua (kupenda kupewa)” .

Muhtasari wa Maana

Al-Mughira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema utajo huu baada ya swala, na yale yaliyohifadhiwa kutoka kwake, rehema na amani ziwe juu yake; ni kuwa amekataza kuongea yasiyofaa, na kuuliza sana yasiyohitajika, na kufuja pesa katika madhambi na israfu katika mambo yanayoruhusiwa, kama vile alivyoharamisha uasi, mauaji ya watoto wa kike, na kuchukua kisichokua chako na kuzuia kile unachopaswa kutoa.

Miradi ya Hadithi