عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ :«عَشْرٌ مِنَ الْفِطْرَةِقَصُّ الشَّارِبِ، وَإِعْفَاءُ اللِّحْيَةِ، وَالسِّوَاكُ، وَاسْتِنْشَاقُ الْمَاءِ، وَقَصُّ الْأَظْفَارِ، وَغَسْلُ الْبَرَاجِمِ، وَنَتْفُ الْإِبِطِ، وَحَلْقُ الْعَانَةِ، وَانْتِقَاصُ الْمَاءِ». قَالَ مُصْعَبٌ: وَنَسِيتُ الْعَاشِرَةَ إِلَّا أَنْ تَكُونَ الْمَضْمَضَةَ

Kutoka kwa Aisha, (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake) amesema:

1- “Mambo kumi ni ya kimaumbile” 

 2- Kukata masharubu, 

 3- kuacha ndevu zikue, 

 4- Kupiga mswaki, 

 5- Kupandisha maji puani, 

 6- Kukata kucha, 

 7- Kuosha nafasi za vidole. 

 8- kunyofoa nywele za kwapa, 

 9- Kunyoa sehemu za siri 

 10- Kustanji”. 

 11- Musab akasema: Nimesahau la kumi ila nahisi ni kusukutua kinywa .

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Mwenyezi Mungu anasema: 

“Na shikeni Swalah na toeni Zaka; na kheri mtakazo jitangulizia nafsi zenu mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yafanya” . 

[Al-Baqarah: 110]

Mwenyezi Mungu alisema: 

“Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi atakaye udiriki mwezi huu naafunge”

[Al-Baqarah: 185]. 

Mwenyezi Mungu amesema:

  “Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo”

[At-Tawbah: 103]. 

Mwenyezi Mungu alisema: 

“Shika Swalah jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima (78) Na amka usiku kwa ibada; ni ziada ya sunna khasa kwako wewe. Huenda Mola wako Mlezi akakunyanyua cheo kinacho sifika” . 

[Al-Isra: 78, 79]

Mwenyezi Mungu alisema:  “Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake” . 

[Al-Baqarah: 184]

Miradi ya Hadithi